Miaka 45 Kuzaliwa kwa chama cha mapindunz Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma ziliamabatanaa na ukaguzi wa Miradi ya uviko 19 ambapo kiwilayaa maadhimisho hayo yalifanyika kata ya Utili Halmashauri ya Mji wa Mbinga. Ikumbukwe maadhimisho hayo yamefanyika kitaifa ktika Mkoa wa Mara manispaa ya Musoma .Kikitiza miaka 45 toka kilipo zaliwa mwaka 1977. Katika maadhimisho hayo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndg Oddo K. Mwisho amesema katika ukaguzi wa miradi hiyo kamati ya siasa ya Mkoa imekuwa ikisisitiza kuwepo na hati miliki, hususani katika taasisi zote za sarikali ili kuepusha migogoro isio ya lazima.
Akitoa hotubayake kwa wananchi na wanachama kata ya utili marabaada ya Uzinduzi wa ujenzi wa ofisi za chama za kata Ndg Mwisho amaesema chama cha mapinduzi bado kinaendelea kujipambanua katika uzalendo wakati kaulimbiu ya maadhimisho hayo ya inasema Chama imara kinaanza na mimi shiriki uchaguzi kwa uadilifu,atahivyo kamatihiyo ya siasa Mkoa imeendea kuwapongeza watumishi na watendaji wa chama na serikali kwa kusimamia kwa uadilifu na Uzalendo miradi mbalimbali inayo endelea katika naeneoyetu.
Kwa upande mwingine mwenyekiti huyo amepongeza hatua ya chama cha mapinduzi Wilaya ya Mbinga kwa kuanza ujezi wa nyumba za jumuhiya mbalimbali katika chama sambamba na uzinduzi wa ugawaji wa vifaa vya kusajili wanachama kwanjia ya kielektroniki hivyo amepongeza sana . Chama cha Mapinduzi mwaka huu kitafanya uchaguzi wa viongozi hivyo kuomba viongozi wanaosimamia uchaguzi kusimamia mafunzo kwa wanachama ili kuwa na uchaguzi wa Amani na utulivu, sambamba na kuwapata viongozi waadilifu na wazuri.
Na Makangury
MBINGA
Sanduku la Barua: P.O.BOX 135
Simu ya Mezani: +225 - 2640664
Mobile: +225 – 2640664
Barua pepe: td@mbingatc.go.tz
Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.