• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga Town Council
Mbinga Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

HALMASHAURI YA WILAYA YA MBINGA NA YA MJI WA MBINGA ZATOA MIKOPO YA SHILINGI BILIONI 2.24 KWA WANANCHI WAKE

Tarehe ya kuwekwa: September 14th, 2023



Na Alex Nelson Malanga


Afisa Habari…MTC


Mbinga:  Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga na ile ya Mji wa Mbinga (MTC) ni sikivu na zinasaidia serikali kuu kuishi ahadi yake ya mikopo itokanayo na fedha za asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri,

 kwa wanawake, vijana  na watu wenye ulemavu.


Kitendo cha kutoa mikopo yenye thamani ya Shilingi bilioni 2.24 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17 hadi 2022/23 huku wanawake wakiwa miongoni mwa wanufaika wakubwa, Halmashauri hizo zinastahili kupewa maua yao.


Hayo yalibainishwa siku ya Jumatano, Septemba 13, 2023 wakati wa Uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Wilaya ya Mbinga katika kata ya Kitula ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Aziza Mangosongo.  


Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Pascar Ndunguru alisema kati ya Shilingi bilioni 2.24, Shilingi bilioni 1.51 zilikwenda Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga na Shilingi milioni 731.58 Halmashauri ya Mji wa Mbinga.


Aliendelea kusema kuwa mikopo hii imetoa fursa za mitaji na uwekezaji kwa vikundi 371 Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga na vikundi 197 Halmashauri ya Mji wa Mbinga.



Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya aliwataka wanawake kuwa na nidhamu ya matumizi ya pesa kwa kutokula mtaji.


“Mtaji ndio nguzo yako. Hata iweje usile msingi wako,” alisema Mhe. Aziza.


Alisema lengo la Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi ni kuwapa ujasiri wanawake katika kujikomboa kiuchumi.


“Tunataka mwanamke aweze kujisimamia mwenyewe na kujitambua,” alisema Mhe. Aziza.


Aliwaambia  wanawake ili wafanikiwe katika biashara wanapaswa kuwa na lugha tamu ili wakonge nyoyo za wateja wao.


Pia alieleza haja ya kufanya biashara katika hali ya usafi ili kuvutia walaji.


Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Mhe. David Mapunda aliipongeza serikali kwa kusimama kidete katika uwezeshaji wanawake kiuchumi.


“ Serikali ina imani kubwa na wanawake kwa kuwa ndio warejeshaji wakubwa wa mikopo,” alisema Mhe. Mapunda.


Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Mkoa wa Ruvuma Bi. Joan Ngapomba alisema mwanzilishi wa Jukwaa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye aliona haja ya kuwa na chombo hicho baada ya kuona wanawake wengi wanapata shida katika kupata mikopo.


“Wakina mama wamekuwa wakipata mikopo ya kausha damu ambayo kwa kweli si rafiki hata kidogo. Tunataka jukwaa hili liwe daraja la akina mama kupata mikopo rafiki kutoka taasisi za kibenki,” alisema Bi. Joan.


Aliwataka wakina mama kuunda vikundi vitakavyowawezesha kupata mikopo kiurahisi.


“Utendaji kazi mzuri, uaminifu na uadilifu ndio utawawezesha wanawake kufaidi huduma ya Jukwaa la Uwezeshaji Kiuchumi,” alisisitiza.


Katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, alieleza Bi. Joan, walifanikiwa kuunda majukwaa 31 katika kata zote na Mbinga Mji majukwaa 19.


Afisa Mahusiano wa NMB Geofrey Maruka aliwakaribisha wajasiriamali wanawake kuchangamkia fursa ya mikopo kutoka benki yao ili waweze kustawisha biashara zao.


Alisema kwa upande wa kilimo benki ya NMB inatoa mikopo kwa wakulima kwa asilimia tisa tuu.



Naye Meneja wa CRDB, Mbinga, Bw. Bedah Mwenda  aliwakaribisha wanawake kujiunga na akaunti za Imbeju na Malkia


Kupitia akaunti hizo, wajasiriamali, hususani walio katika vikundi wataweza kupata mikopo kwa riba nafuu na itakayo wawezesha kutunisha mitaji yao.

Matangazo

  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA June 04, 2025
  • TANGAZO LA KAZI August 07, 2024
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2023 December 14, 2022
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2022 January 04, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kheri ya Siku ya Mazingira Duniani

    June 05, 2025
  • Utoaji wa dawa za minyoo na vitamin A kuanza Juni 1 Mbinga Mji

    May 31, 2025
  • MBINGA MJI YAFANYA TATHIMINI YA LISHE

    May 29, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA WAWASILI MBINGA MJI

    May 26, 2025
  • Tazama zote

Video

MAONYESHO YA NANENANE 2023 MBINGA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.