• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga Town Council
Mbinga Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

MAAFISA UGANI WA MJI WA MBINGA WAKABIDHIWA VIFAA VYA KILIMO VITAKAVYOONGEZA TIJA KWA WAKULIMA

Tarehe ya kuwekwa: September 14th, 2023



Na Elizabeth Newa & Rahma Mwaka


Mbinga. Kilimo ni Uti wa mgongo na ikiwa ni ishara ya kuiishi kauli hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Aziza Mangosongo jana Septemba 13, 2023 alikabidhi vifaa vya Kilimo kwa maafisa Ugani 27 wa kata zote  zilizopo katika Halmashauri ya mji wa Mbinga.


Vifaa hivyo vinavyotarajiwa kuongeza tija katika Kilimo ni Kipima Afya ya Udongo, Bomba za kunyunyizia viwatilifu, Kompyuta, Printa, Lamination mashine, Makoti ya mvua, Buti pamoja na Kishikwambi ambavyo vitawasaidia kufanya kazi kitaalamu na kutunza  takwimu mbalimbali.


Akizungumza wakati wa makabidhiano, Mkuu wa Wilaya alianza kwa kuwakumbusha maafisa ugani kuwa Kilimo ni uti wa mgongo kwani mahitaji mengi ikiwemo  chakula na mavazi yanatokana na Kilimo.


Mhe. Aziza aliishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa Kilimo na kuwapatia vifaa maafisa ugani vitakavyowasaidia kutekeleza majukumu yao ya kuwahudumia wakulima.


Aliishukuru pia Wizara ya Kilimo inayoongozwa na Mhe. Hussein Bashe kwa kutekeleza agizo la kila afisa Kilimo anakuwa na chombo cha usafiri kwa ajili ya kusaidia kazi zao za kila siku na kumpatia kila mmoja  Pampu ya kunyunyizia viwatilifu, Buti za shambani na Koti la mvua.


Akizungumzia kipima udongo, alisema kifaa hicho kitasaidia kupima afya ya udongo katika mashamba ya wakulima ili kujua aina ya udongo na Virutubisho vilivyomo na mazao yanayostawi katika eneo hilo.  


Pia, Mkuu wa Wilaya aliwaagiza maafisa ugani wote kuwa vifaa hivyo vikafanye kazi na kazi ionekane.


“Wakulima wote wapate huduma  ya kupimiwa afya ya udongo katika mashamba yao na kupatiwa vyeti bila malipo yoyote kama ilivyoagizwa na  Mhe. Rais Samia,” alisema Mhe. Aziza.


Alisema kuwa anatambua uzalishaji wa kahawa, maharage na mahindi katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga si mkubwa ikilinganishwa na Halmashauri nyingine.


 Kutokana na uhalisia huo, aliwataka maafisa ugani kwenda kusimamia uzalishaji vizuri ili kuongeza tija na kuwa na manufaa zaidi kwa wakulima.


Kwenye hafla hiyo Mkurugenzi wa Halmashauri  ya Mji wa Mbinga Bi. Amina Seif alishindwa kufika kutokana na kuwa na majukumu mengine ya kitaifa.


Kutokana na sababu hiyo, aliwakilishwa na Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri ya Mji Mbinga Bw. Enock Peter Ndunguru.


Bw. Ndunguru alisema vifaa hivyo walivyopata vitasaidia kupima, kutambua na kuimarisha afya ya udongo.


Alieleza kuwa baada ya kupima udongo mkulima  atapatiwa ushauri wa kitaalamu kulingana na afya ya udongo uliopo katika shamba lake ikiwemo aina ya mbolea itakayofaa katika shamba hilo na kiasi cha mbolea kinachostahili.


Bw. Ndunguru alisema maafisa kilimo pia kupitia vifaa hivyo walivyopatiwa, watawaelekeza wakulima matumizi sahihi ya  pampu pamoja na vipimo vya dawa.


Nae Afisa kilimo  kutoka kata ya Utiri  David Kitalika alisema baada ya kupata kipima udongo wao kama maafisa Kilimo wataenda kuwashauri wakulima kitu ambacho kina uhalisia.


“Uzalishaji katika maeneo mengi ni mdogo kutokana na kukosa vifaa vya kitaalamu na kushindwa kujua ni aina gani ya mbolea inafaa,” alisema Bw. Kitalika.

Matangazo

  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA June 04, 2025
  • TANGAZO LA KAZI August 07, 2024
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2023 December 14, 2022
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2022 January 04, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kheri ya Siku ya Mazingira Duniani

    June 05, 2025
  • Utoaji wa dawa za minyoo na vitamin A kuanza Juni 1 Mbinga Mji

    May 31, 2025
  • MBINGA MJI YAFANYA TATHIMINI YA LISHE

    May 29, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA WAWASILI MBINGA MJI

    May 26, 2025
  • Tazama zote

Video

MAONYESHO YA NANENANE 2023 MBINGA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.