• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga Town Council
Mbinga Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

MBINGA YANUIA KUPUNGUZA AU KUONDOKANA NA UTEGEMEZI

Tarehe ya kuwekwa: August 9th, 2024

 


Mbinga. Ifikapo 2050, Wilaya ya Mbinga ina shauku ya kujiona inapunguza au inaondokana kabisa na utegemezi kutoka Serikali Kuu linapokuja suala la utekelezaji wa bajeti yake.


Shauku hii ilioneshwa siku chache zilizopita wakati wa mkutano uliowaleta pamoja wadau mbalimbali kutoa maoni kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025-2050. 


Kwa mwaka huu wa fedha (2024/25) mchango wa mapato ya ndani ya Halmashauri ya Mji wa Mbinga ni asilimia 10.4 tuu ya bajeti nzima ya Sh31.6 bilioni.


Tafsiri yake ni kuwa utegemezi kwa Serikali kuu ni asilimia 89.6.


Kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mapato ya ndani yanachangia asilimia 17.5 ya bajeti nzima ya Sh48.1 bilioni.


Hii inamaanisha kuwa utegemezi wake kwa Serikali kuu ni asilimia 82.5.


Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Kisare Matiku Makori alisema kuwa ufanisi katika ukusanyaji mapato ya ndani kwa Halmashauri za Mji wa Mbinga na Wilaya ya Mbinga utachochea utoaji huduma bora kwa wananchi.


“Lazima tuzitumie vizuri fursa tulizonazo kama tunataka kuongeza mapato yetu ya ndani,” alisema Mhe. Makori huku akitolea mfano wa mandhari nzuri za Wilaya ya Mbinga jinsi zinavyoweza kuwa kivutio cha watalii.


Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Stuart Kuziwa alielezea haja ya kuendelea kutengeneza mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji ili kuvutia wawekezaji zaidi.


“Tunapaswa kuja na mikakati itakayowapa wananchi na wawekezaji ujasiri wa kuwekeza katika maeneo mbalimbali na hivyo kuongeza makusanyo ya Halmashauri,” alisema Bw. Kuziwa.


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Bw. Joseph Rwiza alisema kuna haja ya wao kupunguza utegemezi kutoka Serikali kuu.


“Kwetu sisi tunaona suluhisho la kupunguza utegemezi kutoka Serikali kuu ni kutengeneza mazingira rafiki ya kuwa na uchumi jumuishi,” alisema Bw. Rwiza.


Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbinga John Ndimbo alisema kama Mbinga inataka kusimama yenyewe lazima ihakikishe inatumia ipasavyo rasilimali zake asilia.


“Tunapaswa kutumia ipasavyo fursa tulizonazo kama tunataka tusiwe wategemezi kwa Serikali kuu,” alishauri Askofu Ndimbo.

Matangazo

  • TANGAZO LA MAJIBU YA USAILI WA UDEREVA MAFUNZO KWA VITENDO June 20, 2025
  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI May 25, 2022
  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA June 04, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 13, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MBINGA MJI APATIWA TUZO

    June 20, 2025
  • MKUTANO WA JUKWAA LA MWAKA LA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI WILAYA YA MBINGA

    June 20, 2025
  • ‎MBINGA MJI YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI

    June 19, 2025
  • ‎JAMII YAHIMIZWA KULINDA HAKI ZA WATOTO

    June 16, 2025
  • Tazama zote

Video

MAONYESHO YA NANENANE 2023 MBINGA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.