• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga Town Council
Mbinga Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

MHE. ALEX ANDOYA ACHAGULIWA KUWA MAKAMU MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI WA MBINGA

Tarehe ya kuwekwa: September 18th, 2023



Na Alex Nelson Malanga


Afisa Habari----MTC


Mbinga.   Ni rasmi sasa Mhe. Alex Andoya, diwani wa kata ya Kilimani, ndiye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga (MTC).


Kama kuna mtu ambaye Ijumaa ya Septemba 15, 2023, ilikuwa ni siku tamu kwake kuliko mtu mwingine yeyote, basi si mwingine bali Mhe. Andoya kwani alipita bila kupingwa katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa  Oddo Mwisho uliopo katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga.


 Hii ina maana kubwa sana kwake kwani ni ishara ya kukubalika na kuaminiwa kwa kiasi kikubwa na madiwani wenzake.


Kukubalika kwake kunathibitishwa na yeye kuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo, huku madiwani wengine wakiamini Mhe. Andoya anatosha na ndio maana alipita kwa kura zote za ndio kutoka kwa wajumbe.  


Mhe. Andoya aliyechaguliwa katika mkutano wa Baraza la Madiwani anachukua nafasi ya Mhe. David Mapunda aliyemaliza muda wake wa mwaka mmoja.    


Madiwani pia walimchagua Mwenyekiti wa Halmashauri, Mhe. Kelvin Mapunda, kuwa mwenyekiti wa kamati ya Fedha, huku Mhe. Batson Mpogolo, ambaye ni diwani wa kata ya Kagugu, akichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya Huduma za Uchumi.


Mhe. Amanyisye Ngonepo, ambaye ni diwani wa kata ya Betherehemu,  alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa Mipango Miji, wakati Mhe. Andoya akivishwa kofia ya pili ya uenyekiti wa kamati ya Kudhibiti Ukimwi.


Kwa upande mwingine, Mhe. Winfrid Komba, diwani wa kata ya Mbambi, alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya Maadili.


Mkutano wa uchaguzi uliongozwa kwa umahiri mkubwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga huku akisaidiwa kwa ukaribu na ustadi mkubwa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi. Amina Seif.          


Akizungumza baada ya uchaguzi Mhe. Mapunda alimtaka makamu Mwenyekiti kufanya kazi kwa weledi mkubwa ili kuipeleka mbele Halmashauri ya Mji wa Mbinga.


“Utaniwakilisha maeneo mbalimbali. Naamini utakuwa mtulivu na mwenye busara ya hali ya juu,” alisema Mhe. Mwenyekiti.


Aliongeza: “Wakuu wa Idara na Vitengo wanakutegemea kwa ushauri wa kina ili mambo yaende.”


Pia alimtaka Mhe. Andoya kusimama kidete katika kumshauri mwenyekiti.


“Ikibidi mimi na wewe tuwe tunaongozana kuelekea kwa Mkurugenzi kuzungumzia mambo muhimu kuhusu mustakali wa Halmashauri yetu,” alisema Mhe. Mapunda.


Kwa upande wake Mkurugenzi Bi. Amina aliwamwamwagia sifa kede kede viongozi waliochaguliwa akiwa na imani kuwa uwezo wao utakuwa chachu ya maendeleo ya Halmashauri.


“Nina imani Makamu Mwenyekiti na viongozi wengine waliochaguliwa kuongoza kamati mbalimbali watakuwa na msaada mkubwa kwa Halmashauri yetu,” alisema Bi. Amina.


Mhe. Andoya, kwa upande wake, alisema yeye na viongozi wenzake watahakikisha wanatimiza majukumu yao kwa kuwapa ushirikiano mkurugenzi, madiwani na wakuu wa idara.


“Nawahakikishia kuwa nipo pamoja nanyi nyote. Nitakuwa daraja la kumshauri Mwenyekiti ili kuhakikisha Halmashauri yetu inasonga mbele,” alisisitiza Mhe. Andoya.

Matangazo

  • TANGAZO LA MAJIBU YA USAILI WA UDEREVA MAFUNZO KWA VITENDO June 20, 2025
  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI May 25, 2022
  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA June 04, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 13, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Wajasiriamali Mbinga Mji washiriki Maonesho ya Sabasaba

    July 08, 2025
  • Mazoezi ya Viungo Mbinga Tc

    July 08, 2025
  • Kheri ya Sikukuu ya Sabasaba

    July 07, 2025
  • Mkurugenzi Halmashauri ya Mbinga Mji atembelea Maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es salaam

    July 05, 2025
  • Tazama zote

Video

MAONYESHO YA NANENANE 2023 MBINGA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.