• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga Town Council
Mbinga Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

MJI MBINGA YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI

Tarehe ya kuwekwa: July 13th, 2024


Na Alex Nelson Malanga


Afisa Habari---Mji Mbinga


Mbinga. Halmashauri ya Mji wa Mbinga iliyopo mkoani Ruvuma imepongezwa kwa kupata hati safi katika mwaka wa fedha 2022/23, huku ikipewa angalizo la kutobweteka.


Pongezi hizo zilitolewa Jumamosi (Julai 13) na viongozi mbalimbali wa serikali wakati wa kikao cha kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa hesabu za Halmashauri ya Mji Mbinga za mwaka wa fedha 2022/23.


Akitoa heko hizo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bi. Rehema Madenge alisema uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga una kila sababu ya kupongezwa.


 “Mnastahili kupewa heko. Lakini hamtakiwi kubweteka na badala yake mnapaswa kukaza buti ili Halmashauri ya Mji wa Mbinga iendelee kupata hati safi,” Bi. Rehema alitoa angalizo.


Katibu Tawala huyo wa Mkoa kwa kiasi fulani alionesha kuridhishwa na Mji Mbinga linapokuja suala la ushughulikiaji wa hoja na mapendekezo ya CAG pamoja na maagizo ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC).


Kwa mujibu wa taarifa ya CAG, kati ya hoja na mapendekezo 26 yaliyotelewa na CAG kwa mwaka wa fedha ulioishia June 30, 2023, yaliyofanyiwa kazi na kufungwa ni mapendekezo 11.


Taarifa inaendelea kueleza kuwa hoja na mapendekezo 15 yapo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.


“Hoja zote zinazostahili kufungwa zitafutiwe majibu na vielelezo kabla au ifikapo Septemba 30 mwaka huu,” aliagiza Bi. Rehema wakati wa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Oddo Mwisho uliopo Mji Mbinga.


Aliongeza: “Utendaji wenu siku zote uzingatie kanuni, sheria na utaratibu ili kuzuia hoja zisijitokeze tena.”


Naye Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Kisare Matiku Makori aliungana na Katibu Tawala wa Mkoa kuipongeza Halmashauri ya Mji Mbinga kwa kupata hati safi.


“Hongereni sana kwa kupata hati safi. Tafsiri ya kupata hati safi ni kwamba tunawajibika ipasavyo katika kusimamia rasilimali zetu,” alisema Mhe. Makori.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Mhe. Kelvin Mapunda aliahidi kushirikiana na wataalamu kuzuia hoja zisizokuwa za lazima na pia kufanyia kazi mapendekezo ya CAG.

Matangazo

  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA June 04, 2025
  • TANGAZO LA KAZI August 07, 2024
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2023 December 14, 2022
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2022 January 04, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kheri ya Siku ya Mazingira Duniani

    June 05, 2025
  • Utoaji wa dawa za minyoo na vitamin A kuanza Juni 1 Mbinga Mji

    May 31, 2025
  • MBINGA MJI YAFANYA TATHIMINI YA LISHE

    May 29, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA WAWASILI MBINGA MJI

    May 26, 2025
  • Tazama zote

Video

MAONYESHO YA NANENANE 2023 MBINGA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.