• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Government Web Framework

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Government Web Framework

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

WAHUDUMU AFYA NGAZI YA JAMII WAPEWE KIPAUMBELE

Tarehe ya kuwekwa: May 23rd, 2024



Na Alex Nelson Malanga


Afisa Habari---Mbinga Mji


Mbinga. Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Kisare Matiku Makori amesema wahudumu wa afya ngazi ya jamii ni nguzo muhimu katika utekelezaji wa afua za lishe na hivyo wanapaswa kupewa kipaumbele linapokuja suala la ajira.


Mhe. Makori jana Mei 22, 2024 aliitaka Halmashauri ya Mji wa Mbinga kuwapa kipaumbele wahudumu hao linapokuja suala la ajira za muda mfano uendeshaji wa kampeni na programu mbalimbali za afya.


Sanjari na hilo, aliitaka Halmashauri hiyo kujenga utamaduni wa kuwaandikia wahudumu wa afya ngazi ya jamii barua za utambuzi ili ziongeze uzito wa wasifu wao na hivyo kuwaweka katika nafasi nzuri zaidi ya kuingia kwenye ajira rasmi pindi nafasi zinapotangazwa.


 “Wahudumu wa afya ngazi ya jamii ni nguzo muhimu katika utoaji wa elimu ya afua za lishe kwani wao ndio wapo karibu zaidi na wananchi,” alisema Mhe. Makori wakati wa kikao cha taarifa ya tathimini ya utekelezaji wa mkataba wa lishe robo ya tatu ya mwaka 2023/24.


Miongoni mwa majukumu yanayofanywa na wahudumu wa afya ngazi ya jamii, ambao huchaguliwa katika ngazi ya kijiji/mtaa kufanya kazi katika maeneo yao husika, ni kutembelea kaya zenye wajawazito ili kuwapatia elimu ya lishe.


Pia, wahudumu hao hutembelea kaya zenye watoto chini ya miaka mitano ili kufuatilia maendeleo ya ukuaji wao na kuwapa wazazi elimu ya unasihi wa lishe na ulishaji wa watoto wadogo na wachanga.


Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Dkt. Kung’e Nyamuryekung’e alisema kuwa wakati wa zoezi la chanjo mbalimbali huwa wanawakumbuka watoa huduma ngazi ya jamii kwa kuwapatia posho.


“Tunataka watu wazingatie afua za lishe ili tujenge jamii yenye afya bora na ndio maana tumekuwa tukiwapatia motisha wahudumu wa afya ngazi ya jamii ili waendelee kutoa elimu kwa wananchi,” alisema Dkt. Nyamuryekung’e.


Afisa Lishe wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Bi. Gloria Maya aliahidi kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala ya urutubishaji wa unga wa mahindi na vyakula vingine kama vile mafuta, unga wa ngano na chumvi.

Matangazo

  • KUITWA KATIKA USAHILI October 13, 2025
  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI May 25, 2022
  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA June 04, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 13, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kambi ya madaktari Bingwa wa Dkt Samia Suluhu Hassan yaendelea kutoa Huduma Halmashauri ya Mji Mbinga

    September 24, 2025
  • KISHINDO CHA MHE.RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN MBINGA MJI KATIKA MIRADI YA ELIMU

    August 29, 2025
  • KISHINDO CHA MHE.RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN MBINGA MJI KATIKA MIRADI YA ELIMU

    August 29, 2025
  • KISHINDO CHA MHE.RAIS,DKT. SAMIA SULUHU HASSAN MBINGA MJI KATIKA MIRADI YA ELIMU

    August 29, 2025
  • Tazama zote

Video

MAONYESHO YA NANENANE 2023 MBINGA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Government Web Framework

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki