• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga Town Council
Mbinga Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

BEI YA UMILIKISHWAJI ARDHI YAPUNGUA KWA ASILIMIA 43

Tarehe ya kuwekwa: October 13th, 2023


Na Rahma Mwaka, Elizabeth Newa & Erasto George.


Mbinga. Maafisa Ardhi wa Wilaya ya Mbinga wamewataka wananchi kuchangamkia fursa ya punguzo la asilimia 42.9 ya bei ya umilikishwaji wa ardhi baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoa ofa hiyo.


 Afisa Ardhi Mteule wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga France Kaganda, alieleza kuwa  kuanzia Julai 1, 2023, gharama zimepungua kutoka Shilingi 163,000  hadi Shilingi 93,000 kwa kiwanja chenye mita za mraba 600.


Bw. Kaganda alikuwa anaongea Oktoba 12, 2023 wakati wa kilele cha kampeni maalum ya siku nne ya kutoa elimu ya masuala yahusuyo usimamizi wa sheria, kanuni na taratibu za uendelezaji wa ardhi, kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi katika Wilaya ya Mbinga.  


"Tunawataka  wananchi wote wenye viwanja ambavyo vimepimwa na vina sifa ya kuandaliwa hati kujitokeza ili kupata nyaraka za hati miliki," alisema  Bw. Kaganda.


Aliongeza kuwa mwananchi akilipa kodi ya ardhi na kupeleka vithibitisho vyote katika idara ya Ardhi, ataandaliwa na kupatiwa hati yake ndani ya siku 14.


Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Aziza Mangosongo aliwataka maafisa Ardhi kutoa hati miliki kwa wakati ili watu waanze shughuli za ujenzi kwa wale wanaohitaji kujenga.


Aliwaasa wananchi kufuata ushauri wa wataalamu wa ardhi ili kuepuka athari mbalimbali zinazoweza kujitokeza baadae ikiwa ni pamoja na kubomolewa nyumba au kupitiwa na mafuriko.


"Watu wengi wamekuwa wakipigana na kuumizana kutokana na migogoro ya ardhi, ninakiagiza kitengo cha Ardhi kuwa wasuluhishi zaidi kuliko kuwa chanzo cha migogoro," aliagiza Mhe. Aziza



Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Bi. Amina Seif alisema kuwaona wataalamu wa ardhi na kupata hati miliki pamoja na ushauri itasaidia kupunguza au kuondoa migogoro ya ardhi.  


“Zoezi hili la kutoa elimu, kusikiliza na kutatua kero za ardhi litakuwa endelevu,” alisema Bi. Amina huku akiomba ushirikiano kwa mkuu wa Wilaya pindi anapopata nafasi.


Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbinga Bi. Pendo Daniel alisema kwa kusikiliza kero kutoka kwa wananchi, itasaidia kupunguza migogoro kwa kiasi kikubwa.


“Nataka zoezi hili liwe endelevu,” aliagiza Bi. Pendo.


Mkuu wa idara ya Ardhi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Bw. John Rikanga alisema idara yake kwa sasa itaongeza nguvu katika kuzuia migogoro ya ardhi ili kupunguza au kuondoa athari za migogoro hiyo.


“Tuzuie migogoro na si kusubiri itokee ndipo tuanze kuitatua,” alisema Bw. Rikanga.


 Alisema migogoro mingi ya ardhi inatokana na mikataba holela ya kuuziana au kukodishiana eneo.


Kwa muktadha huo, alisema kwa wilaya nzima ya Mbinga,  idara itaandaa mkataba wa aina moja wa kuuziana na kukodishiana eneo ili kuwasaidia wananchi kuepuka migogoro ya ardhi.


Katika muda wa siku nne, wananchi 99 walijitokeza kupata elimu na kutoa malalamiko yao ambayo yalitatuliwa mbele ya Mkuu wa Wilaya.

Matangazo

  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA June 04, 2025
  • TANGAZO LA KAZI August 07, 2024
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2023 December 14, 2022
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2022 January 04, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kheri ya Siku ya Mazingira Duniani

    June 05, 2025
  • Utoaji wa dawa za minyoo na vitamin A kuanza Juni 1 Mbinga Mji

    May 31, 2025
  • MBINGA MJI YAFANYA TATHIMINI YA LISHE

    May 29, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA WAWASILI MBINGA MJI

    May 26, 2025
  • Tazama zote

Video

MAONYESHO YA NANENANE 2023 MBINGA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.