Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe Aziza Ally Mangosongo leo amaezindua chanjo ya uviko 19 katika Wilaya hiyo, Wakishiriki Wenyeviti wa Halmashauri hizo Wakuu wa idara na taasisi binafsi, na baadhi wafanya biashara. Atahivyo Mkuu huyo wa Wilaya ametoa maelekezo kwa Viongozi kuzingatiwa katika wimbi la tatu la Uviko 19 na wananchi kwa ujumla. Viongozi wa ngazi zote kuwamfano kwa wananchi kuchua taadhali dhidi ya Uviko 19.Taasisi mbalimbali kuakikishisha zinasimamia watumishi kutekeleza hatua za kuzingatia kujikinga na maambukizi ya Uviko 19 na sio kuleta hofu na kutumia nguvu bali kutoa elimu kwa watumishi.
Taasisi kuakikisha upatikanaji wa vifaa tiba kama barakoa kwa watumishi ,kuwepo na maji tiririka na sabuni pamoja na vipukusa mikono (sanitizer). Vilevile Mkuu huyo ya Wilaya amesisitiza taasisi kupunguza misongamano ya watu sehemu za kazi pasipo kuathili utendeji kazi wa kila siku na shughuli za kiuchumi. Kwa upande mwingine Mhe Aziza amezitaka Halmashauri hizo kuahakikisha maeneo ya uma kama Standi za mabasi ,malori ,Bajaji , Bustani za kupumzika Masoko ,Sehemu za Burudani ,Misikiti na Makanisa yanakuwa na Maji tiririka na sabuni na vinatumika kwa ipasavyo.
Ataivyo Mkuu huyo ameenedela kusisitiza jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kuakikisha mabasi hayasimamishi abilia, na kitengo cha uamiaji kuwachunguza wageni wanaoingia kutumia mipaka yetu itasaidia kuwabaini wageni waliona uviko 19 na kupewa huduma zinazo staihiki kwa wakati . Vituo vya kutolea huduma za afya kama Hospital kupunguza masongamano usio wa lazima kwa ndugu jamaa na marafiki wanaofika kuwaona wagonjwa wao kwa wakati mmoja, angalau afike mmoja ili kuepusha misongamano hiyo.
Katika zoezi hilo la utambulishaji chanjo ya Uviko 19, Mkuu huyo wa Wilaya aliwaongoza viongozi, wa Halmashauri zote, Taasisi Wakuu wa idara na vitengo, baadhi ya madiwani na watendaji kata ,kupata kupata chanjo hiyo . Ataivyo utekelezaji wa upatikanaji wa chanjo, unaendelea kwa kila Halmashauri kuwa vituo ili kurahisisha wananchi kupata chanjo hiyo kwa urahisi. Ikumbukwe chanjo hiyo ni ya hiyari kwa kila mtu, hivyo nujuku la kila mtu kuchukua taadhali dhidi ya Uviko 19
Na Makangury
MBINGA
Sanduku la Barua: P.O.BOX 135
Simu ya Mezani: +225 - 2640664
Mobile: +225 – 2640664
Barua pepe: td@mbingatc.go.tz
Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.