• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga Town Council
Mbinga Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

HALMASHAURI YA MJI WA MBINGA YAFIKIA ASILIMIA 80.4 YA LENGO KATIKA UTOAJI WA KINGA TIBA YA USUBI

Tarehe ya kuwekwa: August 19th, 2023


Mbinga. Katika kipindi cha siku tatu tuu Halmashauri ya Mji wa Mbinga imefikia asilimia 80.4 ya lengo la kuwapatia kinga tiba ya usubi wakazi 126,866 ndani ya siku saba.  


Usubi ni ugonjwa  unaoathiri ngozi na macho ambapo husababisha ngozi kuwasha sana na kuwa ngumu kama mamba, kenge au mjusi na yenye madoadoa kama chui na bila matibabu hupelekea upofu.


Vimelea vya ugonjwa huu huenezwa na nzi wadogo weusi wanaopatikana katika mito inayoenda kwa kasi.


Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Dkt Kung'e Nyamuryekung'e alisema waliopatiwa kinga tiba mpaka leo Agosti 19 ni watu 102,016.


Ili kusema zoezi la kinga tiba ya usubi limefanikiwa inatakiwa kumezesha dawa walau asilimia 80 ya wakazi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga kati ya Agosti 17 zoezi lilipoanza na Agosti 23 siku litakapotamatika.


Tafsiri ya kufikia asilimia 80.4 ya lengo siku ya tatu baada ya zoezi kuanza ni kwamba kuna uwezekano mkubwa Halmashauri ya Mji wa Mbinga ikafikia na hata kuzidi lengo kabla ya siku saba zilizopangwa kumalizika.  


"Zoezi linakwenda vizuri. Mwitiko wa wananchi ni mkubwa tofauti na miaka ya nyuma," alisema Dkt Nyamuryekung'e.


Kwa muda mrefu usubi, ugonjwa maarufu kama River blindness, umekuwa moja ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele na umekuwa ukiathiri sana jamii.


Hiyo ni kwa mujibu wa Mratibu wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele----Halmashauri ya Mji wa Mbinga, Bi Sheila Mbike


Alisema vimelea vya ugonjwa wa usubi huchelewa kujitokeza na kwamba inaweza kuchukua miaka mitano hadi 10.


"Ni vizuri kuchukua tahadhari kwani athari za ugonjwa huu ni kubwa---inaweza kupelekea upofu na hivyo kupunguza nguvu kazi," alisema Bi Sheila.


Kinga tiba ya usubi ni zoezi la kitaifa ambalo hufanyika kila mwaka chini ya Wizara ya Afya katika baadhi ya maeneo yenye maambukizi makubwa.


Kwa Halmashauri ya Mji wa Mbinga, zoezi hilo lilizunduliwa katika Kata ya Mbinga mjini B na Diwani wa kata hiyo Mh Sultan Andoya Alhamisi ya Agosti 17, 2023.


.....na siku ya Ijumaa (Agosti 18), wafanyakazi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga wakiongozwa na  Dkt Nyamuryekung'e, walipata kinga hiyo muhimu ikiwa ni ishara ya kujali afya zao.


Ugonjwa wa usubi umekua pasua kichwa kwa muda mrefu si kwa Tanzania tuu, bali duniani kwote.  


Mnamo Desemba 2015, zaidi ya wajumbe 200 kutoka mataifa 23 barani Afrika pamoja na mashirika ya kimataifa walikutana jijini Kampala, Uganda kujadili mikakati ya kutokomeza ugonjwa wa usubi.


Mpaka kipindi hicho (2015), ugonjwa huo uliathiri watu milioni 120 katika mataifa 35 duniani.


Katika kipindi hicho, barani Afrika pekee angalau watu 800,000 kati ya milioni 31 walioathirika walipoteza uwezo wa kuona.


Na Alex Malanga


Afisa Habari---MTC

Matangazo

  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA June 04, 2025
  • TANGAZO LA KAZI August 07, 2024
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2023 December 14, 2022
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2022 January 04, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kheri ya Siku ya Mazingira Duniani

    June 05, 2025
  • Utoaji wa dawa za minyoo na vitamin A kuanza Juni 1 Mbinga Mji

    May 31, 2025
  • MBINGA MJI YAFANYA TATHIMINI YA LISHE

    May 29, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA WAWASILI MBINGA MJI

    May 26, 2025
  • Tazama zote

Video

MAONYESHO YA NANENANE 2023 MBINGA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.