• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga Town Council
Mbinga Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

HALMASHAURI YA MJI WA MBINGA YAPOKEA BILIONI 11.974 KWAAJILI YA MIRADI YA MAENDELEO

Tarehe ya kuwekwa: January 18th, 2024



Na Alex Nelson Malanga


Afisa Habari---Mbinga TC


Mbinga.  Katika kipindi cha karibia miaka mitatu ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt Samia Suluhu Hassan, Halmashauri ya Mji wa Mbinga imepokea jumla ya Shilingi bilioni 11.974 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.    



Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Bi. Amina Seif alisema hivi karibuni kuwa kiasi hicho kilitumika kutekeleza miradi mbalimbali kwenye sekta za Elimu, Afya, Maendeleo ya jamii, Kilimo, Utawala, Biashara na Mifugo.


Bi. Amina aliyasema hayo katika Manispaa ya Songea wakati wa mkutano uliowaleta pamoja wakurugenzi wa Halmashauri na Manispaa kutoka Mkoa wa Ruvuma kuelezea mafanikio ya uongozi wa awamu ya sita chini ya uongozi wa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan.


“Tuna kila sababu ya kuishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo,” alisema Bi. Amina.



Alisema kuwa Halmashauri katika mwaka wa fedha 2021/2022 ilipokea  jumla ya shilingi bilioni 5.6, mwaka 2022/2023 bilioni 5.4  na mwaka 2023/2024 hadi kufikia mwezi Desemba 2023  Halmashauri ilipokea  shilingi Milioni 974.6.


Katika sekta ya elimu, aliongeza Bi. Amina, kwa kipindi cha miaka mitatu Halmashauri imepokea shilingi bilioni 7.8 kwa ajili utekelezaji wa miradi mbalimbali.


Baadhi ya miradi iliyotekelezwa katika sekta ya elimu ni; Ujenzi wa vyumba vya madarasa 182 , Ujenzi wa shule mpya 4 ambazo ni sekondari ya Lusonga, shule ya msingi Kipika , shule msingi Mpepai na shule ya sekondari Matarawe.


Miradi mingine ni nyumba za walimu 4 katika shule ya sekondari Lusonga  na shule za msingi Pachasita, Miembeni , Ruvuma chini na Kihungu, Ujenzi wa matundu  ya vyoo 186 katika shule mbalimbali za msingi na sekondari na Ujenzi wa vyumba vya maabara 10 katika shule za sekondari Luhuwiko ,Kilimani,Lamata na Kagugu.


Katika sekta ya Afya  kwa kipindi cha miaka mitatu Halmashauri imepokea shilingi bilioni 2 kwaajili utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi  wa vituo viwili vya afya vya Mbangamao na Myangayanga , ujenzi wa zahanati 9  katika vijiji vya Makatani, Matarawe, Kihuka, Lupilo, Njomlole, Mahande na Kitelea.


Katika sekta ya Maendeleo ya Jamii,  kwa kipindi cha miaka mitatu Halmashauri imepokea  na kutumia shilingi bilioni 2.64 kwaajili utekelezaji wa miradi mbalimbali ya uhawilishaji fedha katika kaya maskini na uwezeshaji wananchi kiuchumi.



Wakati kiasi cha shilingi bilioni 2.03 kikitumika katika uhawilishaji wa fedha katika kaya maskini, shilingi  milioni 609.9  imetolewa kwa vikundi 70 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.



Pia Mkurugenzi alisema katika kipindi cha miaka mitatu, Halmashauri ilikusanya na kutumia kiasi cha shilingi bilioni 0.57 kutekeleza miradi katika idara za  kilimo, mifugo,biashara, fedha, Ardhi, mipango na utawala.


 Miradi iliyotekelezwa ni ujenzi wa ofisi za Kata na vijiji, ununuzi wa Pikipiki 27 ,upimaji wa viwanja 2200 na usimamizi na huduma za ushauri kwa wakulima ili kuongeza tija kwa wakulima.

Matangazo

  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA June 04, 2025
  • TANGAZO LA KAZI August 07, 2024
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2023 December 14, 2022
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2022 January 04, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kheri ya Siku ya Mazingira Duniani

    June 05, 2025
  • Utoaji wa dawa za minyoo na vitamin A kuanza Juni 1 Mbinga Mji

    May 31, 2025
  • MBINGA MJI YAFANYA TATHIMINI YA LISHE

    May 29, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA WAWASILI MBINGA MJI

    May 26, 2025
  • Tazama zote

Video

MAONYESHO YA NANENANE 2023 MBINGA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.