• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga Town Council
Mbinga Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

Halmashauri ya Mji wa Mbinga yawataka waendesha bodaboda kuishi kwa upendo na kufuata sheria

Tarehe ya kuwekwa: August 29th, 2023


Na Alex Nelson Malanga

Afisa Habari----MTC


Mbinga. Halmashauri ya Mji wa Mbinga (MTC) imewataka madereva bodaboda kufanya kazi kwa ushirikiano na upendo huku wakifuata kanuni, taratibu na sheria za nchi.

Wito huo ulitolewa Agosti 25, 2023 wakati wa mkutano kati ya viongozi wa Halmashauri hiyo na viongozi wa madereva bodaboda uliofanyika halmashaurini hapo.

Mkutano huo uliitishwa ili kuja na namna bora ya kuwawezesha madereva bodaboda walio kwenye maeneo yasio sahihi kwenda kwenye vijiwe vilivyotengwa kwaajili ya huduma yao.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Mh. Kelvin Mapunda alisema alichogundua ni kukosekana kwa upendo baina ya madereva bodaboda.

Alisema hayo kutokana na baadhi ya madereva hao kusema wanakataliwa kwenye vijiwe vya bodaboda vya mlango wa kutokea na kuingilia stendi, Dapoli na Andoya.

Wanaotakiwa kuhamia vijiwe hivyo mpaka ifikapo Septemba 1, 2023, ni wale wa vijiwe vya  Block A jengo la chini katikati, na Block B jengo la juu katikati.

"Inatakiwa muende vijiwe vya jirani  kupisha maeneo hayo kwaajili ya maegesho ya magari na kupita abiria," alisema mh. Mapunda.

Aliongeza: "Shida ni kwamba hamna ushirikiano. Mnapaswa kupendana. Mnapaswa kushirikiana."

Aliwataka waishi kama ndugu kwani kila mtu anatafuta ridhiki.  

Ipo hoja iliyoibuliwa na baadhi ya madereva bodaboda juu ya ugumu wa wao kuhama kutokana na kuzoea kwenye maeneo yao ya sasa.

Akijibu hoja hiyo, Mh. Mapunda alisema: "Hoja haina mashiko.  Lazima muwe tayari kukubali mabadiliko. Tusiishi kwa mazoea."

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga, Bi Amina Seif, aliwataka madereva bodaboda kutovunja sheria.

Alisema serikali inaongozwa kwa sheria na taratibu na hivyo ni muhimu kuheshimu mamlaka.

" Mnapaswa kupendana na kuoneane huruma katika kazi ," Bi. Amina aliwaasa madereva bodaboda.

Diwani wa Kata ya Mbinga Mjini B Mh. Sultan Andoya  alisema kuondolewa kwa madereva bodaboda katika maeneo tajwa haimaniishi serikali haiwapendi.

"Tunaangalia maslahi mapana ya Taifa....Kitu kinachokuumiza leo, kina faida kwa wanao kesho," alisema Mh. Andoya.

Mwenyekiti wa bodaboda wilaya ya Mbinga Kefase Kamage pia aliwataka madereva bodaboda kutambua kuwa nchi inaongozwa kwa sheria.

"Ni kweli tunatafuta ridhiki lakini lazima tufuate taratibu na sheria za nchi," alisema Kefase.

Matangazo

  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA June 04, 2025
  • TANGAZO LA KAZI August 07, 2024
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2023 December 14, 2022
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2022 January 04, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kheri ya Siku ya Mazingira Duniani

    June 05, 2025
  • Utoaji wa dawa za minyoo na vitamin A kuanza Juni 1 Mbinga Mji

    May 31, 2025
  • MBINGA MJI YAFANYA TATHIMINI YA LISHE

    May 29, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA WAWASILI MBINGA MJI

    May 26, 2025
  • Tazama zote

Video

MAONYESHO YA NANENANE 2023 MBINGA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.