• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga Town Council
Mbinga Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

KAMATI YA FEDHA YA HALMASHAURI YA MJI WA MBINGA YATEMBELEA MIRADI YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 1.003

Tarehe ya kuwekwa: September 2nd, 2023


Na Alex Nelson Malanga

Afisa Habari----MTC


Mbinga. Kamati ya Fedha ya Halmashauri ya Mji wa Mbinga (MTC) inayoundwa na madiwani na wataalamu, jana Septemba 1, 2023, ilikagua utekelezaji wa miradi sita yenye thamani ya Shilingi bilioni 1.003.


Kamati hiyo ikiongozwa na mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Mh. Kelvin Mapunda walianza kwa kutembelea mradi wa Sequip wa Matarawe unaohusisha ujenzi wa shule ya sekondari.


Miradi mingine iliyotembelewa ni ujenzi wa maabara katika sekondari ya Kilimani Kati, Kituo cha afya cha Mbangamao, ujenzi wa madarasa mawili shule ya msingi Mbangamao, ujenzi wa madarasa mawili shule ya msingi Luhangai na ujenzi wa shule mpya kata ya Mpepai.


Mh. Mapunda alisema dhamira ya serikali ni kuboresha huduma kwa jamii.


"Tumedhamiria kusogeza karibu huduma za jamii kwa wananchi wetu" alisisitiza.


Akielezea kuhusu mradi wa Sequip wa Matarawe wenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 560, Mhandisi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Bw. Peter Lupembe alisema mradi huo unahusisha ujenzi wa jengo la madarasa nane, maabara tatu na jengo la utawala


Mradi huo ambao uko kwenye hatua ya msingi, pia unahusisha ujenzi wa jengo la Tehama, maktaba, matundu 10 ya vyoo na kichomea taka.


Kwa upande wake mradi wa ujenzi wa maabara katika sekondari ya Kilimani Kati  wenye thamani ya Shilingi milioni 65, unahusisha ujenzi wa vyumba viwili vya maabara (Fizikia na Biolojia) na ofisi mbili, kwa mujibu wa makamu mkuu wa shule hiyo Bw. Heri Mbunda.


"Mradi huu ambao ulianza kujengwa Februari mwaka huu, uko kwenye hatua za mwisho za utekelezaji," alisema.


Kwa upande mwingine, Afisa Mtendaji wa Kata ya Mbangamao Bw. Bosco Lwoga alisema utekelezaji wa mradi wa kituo cha afya wenye thamani ya Shilingi milioni 500, uko kwenye hatua ya mwisho ya utekekelezaji.


Mradi huu unahusisha ujenzi wa jengo la wazazi na chumba cha upasuaji, maabara, jengo la kufulia, wodi, njia za kuunganisha wodi moja na nyingine, jengo la wagonjwa wa nje (OPD) na ujenzi wa kichomea taka.


Huduma katika kituo hicho cha Afya cha Mbangamao zinatarajiwa kuanza kutolewa ifikapo Septemba 30.


Kwa upande wake mradi wa Shule ya Msingi Mbangamao wenye thamani ya shilingi milioni 53.1, unahusisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu matatu ya vyoo.


Mradi huu uko kwenye hatua ya kuweka sakafu.


Ukija kwenye mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu matatu ya vyoo katika shule ya msingi Luhangai, ujenzi unaendelea vizuri.


Mradi huo unagharimu kiasi cha Shilingi milioni 53.1.


Kamati ya fedha ilihitimisha ziara yake katika mradi wa ujenzi wa shule mpya ya msingi ya Mpepai mkondo wa Mwamko ambapo mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Mapunda alifurahishwa na maendeleo mazuri ya ujenzi.


"Mchakato wa kusajili shule uendelee," aliagiza Mh. Mapunda, huku akimwaga sifa kemkem kwa msimamizi wa ujenzi Bi Fausta Mapunda ambaye ni mkuu wa shule ya msingi Mpepai.


Mradi huo unaogharimu kiasi cha Shilingi  milioni 331.6, unahusisha ujenzi wa madarasa saba ya shule ya msingi na mawili ya awali, kwa mujibu wa Bi  Fausta.


Pia unahusisha ujenzi wa jengo la utawala na vyoo matundu 16, aliongeza Bi. Fausta.

Matangazo

  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA June 04, 2025
  • TANGAZO LA KAZI August 07, 2024
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2023 December 14, 2022
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2022 January 04, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kheri ya Siku ya Mazingira Duniani

    June 05, 2025
  • Utoaji wa dawa za minyoo na vitamin A kuanza Juni 1 Mbinga Mji

    May 31, 2025
  • MBINGA MJI YAFANYA TATHIMINI YA LISHE

    May 29, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA WAWASILI MBINGA MJI

    May 26, 2025
  • Tazama zote

Video

MAONYESHO YA NANENANE 2023 MBINGA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.