• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Government Web Framework

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Government Web Framework

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

KAMATI YA LISHE YATAKIWA KUSHIRIKIANA NA IDARA MTAMBUKA KATIKA USIMAMIZI WA SHUGHULI ZA LISHE

Tarehe ya kuwekwa: October 29th, 2023


Na Erasto George & Rahma Mwaka


Mbinga. Kaimu Mkurugenzi wa Halmaushauri ya Mji wa Mbinga Dkt. Kung’e Nyamuryekung’e ameitaka kamati ya Lishe ya Halmashauri hiyo  kushirikiana na idara mtambuka katika usimamizi wa shughuli mbalimbali za lishe katika jamii.


Dkt. Nyamuryekung’e alitoa wito huo katika kikao cha kamati ya Lishe ya Halmashauri hiyo kilichofanyika Oktoba 26, 2023 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Mbinga kujadili taarifa ya utekelezaji wa shughuli za lishe robo ya kwanza 2023/24.


Alisema idara mtambuka kama Mipango, Utumishi, Kilimo, Maendeleo ya Jamii, Elimu na Viwanda na Biashara, zinapaswa kutambua kuwa ni jukumu lao kwa kushirikiana na idara ya huduma za Afya,ustawi wa jamii na Lishe, kuhakikisha  wananchi wanapata lishe bora.


“Lishe ndio kila kitu kwenye mwili wa binadamu. Tusiache kutengeneza kompozisheni ya usimamizi wa shughuli za masuala ya lishe zitakazo jumuisha wataalamu kutoka idara mtambuka ,” alisisitiza Dkt. Nyamuryekung’e.


Afisa lishe wa Halmashauri ya Mji Mbinga Gloria Maya aliiomba idara ya elimu kupita kwenye shule kuhamasisha haja ya kuwa na bustani za mbogamboga, klabu za lishe na kuhakikisha wanafunzi wanakula vizuri.


Aidha, Bi. Gloria aliwaomba idara ya Viwanda kusaidia kufunga mashine za kuongeza virutubisho kwenye unga wa mahindi na kuhamasisha wawekezaji kuongeza viinilishe ili kuwe na idadi kubwa ya mashine zinazoweza kuongeza viinilishe.



“Pia tumeongea na mdau wa SANKU  ili atusaidie kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kutumia unga wenye viinilishe,’’alisema Gloria


SANKU ni mtoa huduma katika programu ya kuchanganya virutubishi kwenye unga wa mahindi.


Afisa lishe mwingine wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga, Bw. Martin Kwimba, ndiye aliyewasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za lishe robo ya kwanza na kusoma maazimio ya tathimini ya  kikao cha lishe cha wilaya kilichofanyika Oktoba 19, 2023.



Bw. Kwimba alisema katika kikao cha lishe ngazi ya wilaya  kulikuwa na maazimio kadhaa yaliyofikiwa ikiwemo shule zote kuwa na klabu za lishe na kuhakikisha utekelezaji wa siku ya Afya na Lishe ya kila mtaa/kijiji.


Maazimio mengine ya kamati  ya Lishe ya Wilaya, Bw. Kwimba aliongeza, ni pamoja na kuhakikisha kunakuwepo usimamizi mzuri wa chakula kinachochangiwa na wazazi shuleni.

Matangazo

  • KUITWA KATIKA USAHILI October 13, 2025
  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI May 25, 2022
  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA June 04, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 13, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kambi ya madaktari Bingwa wa Dkt Samia Suluhu Hassan yaendelea kutoa Huduma Halmashauri ya Mji Mbinga

    September 24, 2025
  • KISHINDO CHA MHE.RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN MBINGA MJI KATIKA MIRADI YA ELIMU

    August 29, 2025
  • KISHINDO CHA MHE.RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN MBINGA MJI KATIKA MIRADI YA ELIMU

    August 29, 2025
  • KISHINDO CHA MHE.RAIS,DKT. SAMIA SULUHU HASSAN MBINGA MJI KATIKA MIRADI YA ELIMU

    August 29, 2025
  • Tazama zote

Video

MAONYESHO YA NANENANE 2023 MBINGA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Government Web Framework

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki