• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga Town Council
Mbinga Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

KATA YA MASUMUNI YAIBUKA MSHINDI MASHINDANO YA USAFI MJI WA MBINGA

Tarehe ya kuwekwa: September 11th, 2023


Na Alex Nelson Malanga


Afisa Habari-----MTC


Mbinga.  Wakazi wa Kata ya Masumuni katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga (MTC) wana kila sababu ya kutabasamu baada ya kuibuka washindi wa mashindano ya usafi katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga kwa kuzishinda kata nyingine saba.


Kata hiyo ilitangazwa mshindi jana Septemba 10, 2023 na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Aziza Mangosongo wakati wa kilele cha kampeni ya usafi ijulikanayo kama Mangosongo Oparesheni Safisha Mji: Mbinga ing’ae.


Kata hiyo ya Masumuni ilikabidhiwa fedha taslimu Shilingi 100,000, na mbuzi mweupe ikiwa ni ishara ya usafi.


Mshindi wa pili na watatu ni kata ya Matarawe na Ruhuwiko, kwa mtiririko huo.


Wakati Matarawe wakipata Shilingi 100,000 kama zawadi, Ruhuwiko walipata Shilingi 50,000.



Kata ya mwisho kwa usafi na ambayo usafi wake hauridhishi ni Mbambi ambayo ilipewa hati ya onyo huku Mkuu wa Wilaya akiwataka watendaji wa Kata na Mitaa wabadilike.


Aliitaka Kata hiyo kurudia usafi kuanzia leo Septemba 11, 2023 hadi Jumapili Septemba 17, 2023.


Katika ngazi ya Taifa, kampeni ya usafi ilianzishwa na viongozi wa kitaifa wakiongozwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, baada ya kuona hali ya usafi katika baadhi ya maeneo si ya kuridhisha.


Viongozi hao waliamuru usafi kufanyika kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi.



“Mheshimiwa Rais amekuwa akituhimiza kila mara kuhakikisha maeneo yetu ni masafi. Sisi kama Mbinga tumeamua kufanya kwa vitendo,”


Kampeni hii iliyotamatishwa jana itakuwa ikifanywa kila baada ya miezi mitatu.


Tafsiri yake ni kwamba itazinduliwa tena mwezi wa kumi na mbili.


Akizungumza kabla ya kupata dharura na kuondoka, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Bi. Amina Seif alisema ni vema jamii ikatambua kuwa uchafu wa mazingira ni sababu kuu ya maradhi duniani kwote.



“Kinachotakiwa ni kila mmoja wetu kama mwananchi kuhakikisha kuwa anasafisha mazingira yanayomzunguka na kuelimisha wale ambao hawajui umuhimu huo,” alisema Bi. Amina.


Viongozi wengine waliohudhuria bonanza la jana ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbinga Bi. Pendo Daniel, madiwani wa kata mbalimbali na wakuu wa vitengo kutoka ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Halmashauri ya Mji wa Mbinga.

Matangazo

  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA June 04, 2025
  • TANGAZO LA KAZI August 07, 2024
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2023 December 14, 2022
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2022 January 04, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kheri ya Siku ya Mazingira Duniani

    June 05, 2025
  • Utoaji wa dawa za minyoo na vitamin A kuanza Juni 1 Mbinga Mji

    May 31, 2025
  • MBINGA MJI YAFANYA TATHIMINI YA LISHE

    May 29, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA WAWASILI MBINGA MJI

    May 26, 2025
  • Tazama zote

Video

MAONYESHO YA NANENANE 2023 MBINGA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.