Kiongozi wa Mbio maalum za Mwenge wa Uhuru mwaka 2021 Lt. Josephine P. Mwambashi amezipongeza Halmashauri za Wilaya ya Mbinga kwa usimamizi na utekelezaji mzuri wa miradi yote ya maendeleo iliyotembelewa na Mwenge huo. Mwenge maalum wa Uhuru umekimbizwa Wilayani Mbinga marabaada ya kupokelewa katika kijiji cha Mkako alfajili ya tarehe 4 Septemba2021 ukitokea Wilaya ya Namtumbo na kukabidhiwa leo Septemba 5 Wilayani Nyasa katika Kijiji cha Mkalole ambapo ukiwa Wilayani Mbinga umetembelea jumla ya miradi nane yenye thamani yaTshs. Bilioni 3.14 kutoka Halmashauri zote mbili za Wilaya na Mji wa Mbinga.
Akikabidhi Mwenge maalumu wa Uhuru leo tarehe 5 Septemba 2021 kwa Halmashauri Wilaya ya Nyasa Mkuuwa Wilaya ya Mbinga Mhe: Aziza Ally Mangosongo amesema miradi iliyopitiwa na Mwenge maalumu wa Uhuru katika Wilaya ya Mbinga ni kuwekajiwe la msingi Mradi wa ujenzi wa tenki la Maji Lusaka ambapo kukamilika kwa mradihuo kutaghalimu Tshs.Bilioni 1.41 , kufunguliwa kwa kituo cha Redio Hekima FM, ufunguzi wa Nyumba ya Mkurugenzi wa Mji ambayo imeghalimu Tshs; Milioni 300, pamoja na mradi wa Barabara ya Lami ya Mbuyula inayotekelezwa na Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini TARURA Wilaya ya Mbinga ukighalimu kiasi cha Tshs.Milioni 553.8.
Amesema Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga imetembelewa na miradi ya Klabu ya wapinga rushwa shule ya wasichana Mbinga ,jengo la Udhibiti ubora wa Elimu lenye thamani yaTshs.Milioni 181.8 ambaloli mezinduliwa. Pia kuweka jiwe la msingi katika ujenziwa Hospitali ya Halmashauri ambao unataraji kughalimu kiasi cha Tshs. Milioni 500 katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wake unaotarajiwa kukamilika Disemba mwaka huu 2021.
Atahivyo Kiongozi wa Mbio maalum za Mwenge Lt. Josephine P.Mwambashi amekagua Kikundi cha Vijana cha Chipukizi kinachojishughulisha na ufyatuajiwa tofali za zege ambacho pia nimoja kati ya vikundi vilivyowezeshwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kupitia mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri hiyo kwakupatiwa mkopo waTshs. Milioni 22 kwa mwaka wa fedha 2020/2021. Luteni Mwambashi amewapongeza sana Wilaya ya Mbinga kwa kukubaliwa miradi yote iliyotembelewa na Mwenge maalumu wa Uhuru, hivyo amesistiza kuendelea kusimamia miradi inayoendelea na ujenzi na kuhakikisha inamalizika kwawakati
Na Makangury
MBINGA
Sanduku la Barua: P.O.BOX 135
Simu ya Mezani: +225 - 2640664
Mobile: +225 – 2640664
Barua pepe: td@mbingatc.go.tz
Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.