Baraza la Madiwani Halmashauri ya mji wa mbinga, limepitisha rasimu ya mpango wa bajet kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kiasi cha Tsh ; Bilion 25.34, akisoma rasimu hiyo afisa mipango wa Halmashuri hiyo Ndg Donald Msigwa amesema bajeti hiyo ni ongezeko la asilimia 8.3 ambapo awali makadirio kwa mwaka wa fedha 2021 yalikuwa Bilioni 23.38. Atahivyo madiwani hao wameshauri baraza hilo kuongeza vyanzo vya mapato ikiwemo mizani kwakuwa biashara nyingi za ubebaji wa mizigo zimekuwa zikifanyika na kupita katika maeneo hayo hususani biashara ya ubebaji wa mbao, mazao mbalimbali na makaa ya mawe kutoka Nyasa
Kwaupande wake Mbunge wa Mbinga Mjini Mhe Jonas Mbunda amewapongeza madiwani hao kwa kuonyesha nia ya kuongeza vyanzo vya ukusaji wa mapato, ambapo amaesaema kwa kufanya hivyo kutasaidia kuipanga bajeti katika Halmashauri hiyo, hivyo akaomba madiwani kupewa muda wa kujadili vyanzi vya mapato ili wafikapo katika vikao vya bajeti waweze kuchakata bajeti kwa ufasaa
Na Makangury
MBINGA
Sanduku la Barua: P.O.BOX 135
Simu ya Mezani: +225 - 2640664
Mobile: +225 – 2640664
Barua pepe: td@mbingatc.go.tz
Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.