• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Government Web Framework

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Government Web Framework

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

MAMBO TISA KUTAWALA SIKU YA WAZEE DUNIANI KATIKA HALMASHAURI YA MJI WA MBINGA

Tarehe ya kuwekwa: September 25th, 2023


Na Rahma Mwaka, Elizabeth

Newa & Erasto George



Mbinga. Kamati ya maandalizi ya maadhimisho ya siku ya wazee duniani ya Halmashauri ya Mji Mbinga imesema mambo tisa yatafanyika kuelekea, na wakati wa maadhimisho ya siku hiyo itakayofanyika Oktoba 1 mwaka huu.      


Mambo hayo ni kutoa huduma za afya yakiwemo matibabu, vipimo na elimu lishe kwa wazee, kutoa msaada wa kisaikolojia na kijamii kwa wazee na wananchi wenye uhitaji na kuelimisha jamii kuhusu  masuala ya maadili na ukatili, kwa mujibu wa Afisa Ustawi wa Halmahauri ya Mji wa Mbinga Bw. Lucas Muhina.


Pia, Bw. Muhina aliyekuwa anaongea wakati wa kikao cha kwanza cha maandalizi wiki iliyopita aliongeza kuwa kamati itaandaa mabanda ya maonyesho kuhusu huduma za ustawi kwa wazee na kutoa elimu kuhusu huduma za ustawi wa jamii hususani kwa wazee katika vyombo vya habari na mikutano.


“Sanjari na hayo, wadau watajadili namna bora ya kutatua changamoto za wazee, kudhibiti mmomonyoko wa maadili na ukatili wa kijinsia, na kupata shuhuda za vitendo vya ukatili dhidi ya wazee vilivyowahi kutokea katika maeneo mbalimbali,” alisema Bw. Muhina.  


Pia siku hiyo inatarajiwa kupambwa na michezo mbalimbali itakayowahusisha wazee ikiwemo kukimbia, kuvuta kamba, kukimbiza kuku na kucheza muziki.


Na mwisho wa siku, maafisa ustawi watawatunuku vyeti vya utambuzi wazee waliofanya vizuri katika jamii kama ilivyoagizwa na ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa.


Kikao cha kwanza cha maandalizi ya siku ya wazee kiliongozwa na mwenyekiti Lusiana Ndunguru na katibu Bw. Paul Mbawala ambaye ni mkuu wa huduma za Ustawi wa mji wa Mbinga.


Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Oddo Mwisho kilihudhuriwa na Afisa Utamaduni wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga, maafisa ustawi kutoka Wilaya ya Mbinga  na wajumbe 5 waliowawakilisha wazee.

Matangazo

  • KUITWA KATIKA USAHILI October 13, 2025
  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI May 25, 2022
  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA June 04, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 13, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kambi ya madaktari Bingwa wa Dkt Samia Suluhu Hassan yaendelea kutoa Huduma Halmashauri ya Mji Mbinga

    September 24, 2025
  • KISHINDO CHA MHE.RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN MBINGA MJI KATIKA MIRADI YA ELIMU

    August 29, 2025
  • KISHINDO CHA MHE.RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN MBINGA MJI KATIKA MIRADI YA ELIMU

    August 29, 2025
  • KISHINDO CHA MHE.RAIS,DKT. SAMIA SULUHU HASSAN MBINGA MJI KATIKA MIRADI YA ELIMU

    August 29, 2025
  • Tazama zote

Video

MAONYESHO YA NANENANE 2023 MBINGA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Government Web Framework

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki