• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga Town Council
Mbinga Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

MATOKEO YA SENSA CHACHU YA MAENDELEO

Tarehe ya kuwekwa: April 18th, 2024


Na Alex Nelson Malanga


Afisa Habari---Mbinga Mji


Mbinga.  Halmashauri ya Mji wa Mbinga imedhamiria kutumia sensa ya watu na makazi ya 2022 katika kuratibu mipango ya maendeleo kisayansi na hivyo kusogeza huduma za kijamii karibu zaidi kwa wananchi.


 Hayo yalisemwa Aprili 16, 2024 na viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Mbinga wakati wa mafunzo ya matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kwa viongozi, watendaji, makundi na wadau mbalimbali.


Akifungua mafunzo hayo yaliyotolewa na maofisa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Kisare Matiku Makori aliwataka viongozi katika ngazi mbalimbali wilayani kwake kutumia takwimu za sensa katika kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo.


“Hizi takwimu tusizione kama mapambo….tuzitumie katika kupanga mipango ya maendeleo ya watu wetu ili wanufaike na rasilimali za nchi hii kama Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alivyojidhatiti kipindi anaingia madarakani mwaka 2021,” alisema.


Akiwapatia chakula cha ubongo washiriki wa mafunzo, mtaalamu kutoka NBS Dkt. Mwinyi Mwinyi alisema kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2022, Halmashauri ya Mji wa Mbinga ina jumla ya watu 158,896.


Kati ya watu hao, alielezea, wa jinsi ya kike ni 83,014 na wakiume ni 75,882.


Katika kata 19 za Halmashauri ya Mji wa Mbinga, Mpepai ndiyo inaongoza kwa kuwa na watu wengi zaidi ambao ni 17,072 na Mbinga Mjini B ndiyo yenye watu wachache zaidi, 3,160.



Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Mhe. Alex Andoya alisema: “Tutatumia takwimu hizi katika kutekeleza miradi ya maendeleo na kwa kufanya hivyo miradi hii italeta tija kubwa kwa wananchi wetu”


Mhe. Andoya ambaye pia ni diwani wa kata ya Kilimani, aliungwa mkono na Mbunge wa Mbinga Mjini Mhe. Jonas Mbunda.


Mhe. Mbunda alisema kabla ya kupeleka mradi wa maendeleo eneo husika ni lazima idadi ya watu ifahamike kwa lengo la kuleta tija kwa jamii.


Alikwenda mbali zaidi na kusema kuwa kupitia matokeo ya sensa ya 2022, Halmashauri ya Mji wa Mbinga itaweza kuainisha maeneo mapya ya biashara na vyanzo vipya vya mapato.


Alihitimisha kwa kusema: “Sensa ina umuhimu kwa kila kitu tunachotaka kufanya kwenye jamii.”

Matangazo

  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA June 04, 2025
  • TANGAZO LA KAZI August 07, 2024
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2023 December 14, 2022
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2022 January 04, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kheri ya Siku ya Mazingira Duniani

    June 05, 2025
  • Utoaji wa dawa za minyoo na vitamin A kuanza Juni 1 Mbinga Mji

    May 31, 2025
  • MBINGA MJI YAFANYA TATHIMINI YA LISHE

    May 29, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA WAWASILI MBINGA MJI

    May 26, 2025
  • Tazama zote

Video

MAONYESHO YA NANENANE 2023 MBINGA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.