• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga Town Council
Mbinga Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

Mdaka: TUWEKEZE KATIKA KUZUIA UKATILI WA KIJINSIA

Tarehe ya kuwekwa: December 11th, 2023


Na Alex Nelson Malanga


Afisa Habari----MTC


Mbinga.  Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Mbinga Bw. Joseph Augustino Mdaka amewataka wakazi wa wilaya hiyo kuwekeza zaidi katika kuzuia vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.


Alitoa wito huo jana (Disemba 10, 2023) wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yaliyofanyika katika kijiji cha Mzuzu, Kata ya Kitura.


 “Wanawake na watoto ni kundi linalopitia changamoto zaidi za ukatili wa kijinsia kutokana na uwepo wa mila na desturi kandamizi,” alisema Bw. Mdaka wakati wa maadhimisho yaliyokwenda kwa kauli mbiu: Wekeza kuzuia ukatili wa kijinsia.



Aliwapongeza wadau wote wanaoshughulika na kuibua vitendo vya ukatili kwani jitihada zao zinasaidia sana kubaini na kupunguza vitendo vya kikatili katika jamii.


Aidha, alisema suala la kushughulikia ukatili wa kijinsia ni jukumu la kila mmoja.


“Kila mmoja wetu awe balozi kwa nafasi yake,” alisema Bw. Mdaka.


Uwepo wa vitendo vya ukatili, alisema, umekuwa na athari kubwa katika kujenga mahusiano mema katika jamii na hivyo kupelekea kuporomoka kwa maadili na kushuka kwa uchumi katika kaya na jamii kwa ujumla.


Aliongeza kuwa jamii imeshuhudia kukua kwa utegemezi kwenye familia na ongezeko la watoto wa mitaani waliopoteza matumaini na upendo kutoka kwa wazazi wao.


Matokeo ya uwepo wa kizazi hiki ni kutengeneza kundi la wezi na ‘panyarodi’ ambao wanafanya jamii kuishi kwa mashaka.


Alitoa rai kwa viongozi katika ngazi ya vijiji, mitaa na kata kutoa ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha vitendo vya ukatili wa kijinsia vinafichuliwa na kuripotiwa katika vyombo vya sheria.


“Mkitakiwa kutoa ushahidi, hamna budi kutoa ushirikiano wa kutosha,” alisema.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Bi. Amina Seif alitoa msisitizo kwa wanajamii kuibua na kufichua matukio yote ya ukatili wa kijinsia yanayoendelea kuanzia katika ngazi ya familia.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Bw. Juma Haji Juma alielezea haja ya kutengeneze mazingira ya upendo kwenye familia ili kuepukana na vitendo vya kikatili ambavyo vinakwamisha maendeleo katika jamii.  


Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni  ya kimataifa ya kupinga ukatili  dhidi ya wanawake.


 Kampeni hii hufanyika kuanzia Novemba 25 na kumalizika Disemba 10  ya kila mwaka kwa ajili ya kupinga ukatili na kutetea haki za wanawake.

Matangazo

  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA June 04, 2025
  • TANGAZO LA KAZI August 07, 2024
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2023 December 14, 2022
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2022 January 04, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kheri ya Siku ya Mazingira Duniani

    June 05, 2025
  • Utoaji wa dawa za minyoo na vitamin A kuanza Juni 1 Mbinga Mji

    May 31, 2025
  • MBINGA MJI YAFANYA TATHIMINI YA LISHE

    May 29, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA WAWASILI MBINGA MJI

    May 26, 2025
  • Tazama zote

Video

MAONYESHO YA NANENANE 2023 MBINGA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.