• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga Town Council
Mbinga Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

MHE. MAKORI: MARUFUKU KUCHEZEA MASLAHI YA WAKULIMA

Tarehe ya kuwekwa: August 6th, 2024


Na Alex Nelson Malanga


Afisa Habari----Mji Mbinga.


Mbinga.  Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Kisare Matiku Makori amesema serikali haitakuwa tayari kuona maslahi yanayohusiana na wakulima yanachezewa kwa namna yoyote ile.


Mhe. Makori aliyasema hayo siku ya Jumanne (Agosti 6) kufuatia kuwepo kwa malalamiko dhidi ya baadhi ya Vyama vya Ushirika katika wilaya yake kupora haki za wakulima.


Alisema kati ya malalamiko anayopelekewa ofisini kwake, masuala yanayohusiana na vyama vya ushirika yanashika namba moja huku akisema kilio cha  wakulima ni ukomo wa madeni na malipo ya awamu ya pili.


“Hii haikubaliki, lazima tulisimamie kwa ukaribu” Mhe. Makori alisema wakati wa mkutano na kamati ya siasa ya Mkoa wa Ruvuma uliofanyika katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga chini ya mwenyekiti wa CCM-Mkoa wa Ruvuma Bw. Oddo Mwisho.


Mhe. Makori alisema kuwa tayari amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri za Mji wa Mbinga na Wilaya ya Mbinga wawaandikie maafisa ushirika na viongozi wote wa vyama ushirika nini cha kufanya kuhusu ukomo wa madeni na malipo ya wakulima.


 “Nimewataka wawaandikie kuwa hakutakuwa na uidhinishwaji wa ukomo wa madeni na hakutakuwa na malipo ya wakulima kwenye vyama vya msingi bila taarifa kufika ofisi ya mkurugenzi,” alisema.


 Aliongeza: “Na baada ya kufika ofisi ya mkurugenzi, wakaguzi wa ndani wa Halmashauri watapaswa kufanya ukaguzi.”


Kwa mujibu wa Mhe. Makori, kati ya vyama vya ushirika 120 vilivyopo katika mkoa wa Ruvuma, 100 vipo wilaya ya Mbinga.


Alikwenda mbali kufafanua kuwa kati ya vyama hivyo 100 vilivyopo Wilaya ya Mbinga, vyama 21 vipo Halmashauri ya Mji wa Mbinga na 79 Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.


 “Wilaya ya Mbinga iko vizuri katika kilimo cha mahindi na kahawa---ukicheza kidogo na maslahi yanayohusiana na wakulima, utakuwa umetikisa msingi wa uchumi wa wananchi wa Wilaya hii,” alihitimisha Mhe. Makori.


 Mkutano wa Jumanne uliwaleta pamoja viongozi wa CCM ngazi ya Wilaya na Mkoa, wataalamu wa Halmashauri za Mji wa Mbinga na Wilaya ya Mbinga pamoja na wakuu wa taasisi za wilaya ya Mbinga.

Matangazo

  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA June 04, 2025
  • TANGAZO LA KAZI August 07, 2024
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2023 December 14, 2022
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2022 January 04, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kheri ya Siku ya Mazingira Duniani

    June 05, 2025
  • Utoaji wa dawa za minyoo na vitamin A kuanza Juni 1 Mbinga Mji

    May 31, 2025
  • MBINGA MJI YAFANYA TATHIMINI YA LISHE

    May 29, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA WAWASILI MBINGA MJI

    May 26, 2025
  • Tazama zote

Video

MAONYESHO YA NANENANE 2023 MBINGA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.