• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga Town Council
Mbinga Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

MJI WA MBINGA WANG’AA BAADA YA KUTAMATIKA KWA KAMPENI YA MANGOSONGO OPARESHENI SAFISHA MJI: MBINGA ING'AE

Tarehe ya kuwekwa: September 11th, 2023


Na Alex Nelson Malanga


Afisa Habari---MTC


Mbinga. Mji wa Mbinga umetakata, mji wa Mbinga unang’aa, Mji wa Mbinga unameremeta, hivyo ndivyo unavyoweza kusema, shukrani kwa kampeni ya usafi ijulikanayo kama Mangosongo Oparesheni Safisha Mji: Mbinga ing’ae.


Kampeni hiyo ambayo ni zao la Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Aziza Mangosongo, ilianza September 4 na kutamatika Jana, September 10.


Akizungumza wakati wa kilele cha kampeni hiyo katika uwanja wa Sekondari Makita, Mhe.Mkuu wa wa Wilaya alisema kabla ya kuanza kwa kampeni hali ilikuwa mbaya---takataka zilizagaa mtaani, vichaka vilikuwa vingi hasa kwenye maeneo ya taasisi na maeneo ya kuzunguka nyumba za watu.


“Sasa hivi ukipita maeneo ya sokoni, mitaani na barabara kuu hakuna taka wala nyasi,”alisema Mhe. Mangosongo.


Aliongeza: “Natoa wito, desturi hii ya kufanya usafi iendelee bila kusimamiwa.”


Aliwataka wamiliki wote wa bustani zilizochini ya Halmashauri ya Mji wa Mbinga wazihudumie na wakishindwa zirejeshwe kwa mamlaka husika ili wapewe watu wengine.


Alihimiza ujenzi wa vyoo bora katika makazi ya watu na sehemu za starehe.


Hili, aliongeza, liende sanjari na kuweka mazingira safi ya vyoo hivyo.


“Katika maeneo ya starehe (baa), kuwe na muhudumu wakupita mara kwa mara kuhakikisha vyoo ni visafi,”aliagiza Mhe. Mangosongo.


Alitoa miezi mitatu kwa maeneo ambayo vyoo vimejaa vijengwe vipya.


Kwa vyoo vilivyojengwa kwa nyasi au makuti aliamuru viondolewe na vijengwe vya kisasa.


Alisema zoezi la usafi litaendelea kila Jumamosi ya wiki mpaka pale atakaporidhishwa na usafi wa mazingira maeneo yote.


“Tunafunga kampeni hii leo (jana) lakini zoezi la usafi linaendelea,”alisema Mhe. Mangosongo.


Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Wilaya, kampeni hii itakuwa ikifanywa kila baada ya miezi mitatu.


Tafsiri yake ni kwamba itazinduliwa tena mwezi wa kumi na mbili.


Pamoja na usafi wa mazingira, Mhe. Mangosongo aliwataka wakazi wa Mbinga wawe wasafi  wa roho pia.


“Mnapaswa kuwa na moyo safi usio na kinyongo wala makandokando,”alishauri.


Alihitimisha kwa kunukuu kifungu cha biblia kutoka Mathayo Mtakatifu 5: 8:“Heri wenye moyo safi, maana hao watamwona Mungu.”


 Pamoja na Mkuu wa Wilaya, bonanza la usafi lilihudhuriwa na viongozi wengine ambao ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbinga Bi. Pendo Daniel na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga (MTC) Bi. Amina Seif, ambaye baadaye alipatwa na dharura na hivyo kukaimisha  nafasi hiyo kwa Dkt Kung’e Nyamuryekung’e.


Wengine waliohudhuria ni madiwani wa Kata mbalimbali, wakuu wa idara kutoka ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Halmashauri ya Mji wa Mbinga pamoja na watendaji wa Kata na Mitaa.


Akizungumza kabla ya kuondoka katika bonanza hilo Bi. Amina alisema usafi wa mazingira ni muhimu katika mapambano dhidi ya maradhi.


Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), upungufu wa usafi wa mazingira ni sababu kuu ya kuenea kwa maradhi duniani.


“Usafi wa mazingira una manufaa makubwa sana. Si wakati wa kuchekea uchafuzi wa mazingira,” alisema Bi. Amina.


Akizungumza baada ya Mkurugenzi kuondoka, Kaimu Mkurugenzi Dr Nyamuryekung’e alisema usafi wa mazingira ni muhimu sana ili kuhakikisha kuwa afya inazingatiwa na kuzuia uwezekano wa binadamu kukabiliana na athari za taka.


Afisa Afya wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Felix Matembo alisema: “Tunawajibu kama Serikali kuhakikisha kuwa wananchi wanaishi katika mazingira mazuri. Wananchi nao wafanye sehemu yao badala ya kusubiri kila kitu kutekelezewa na serikali.”

Matangazo

  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA June 04, 2025
  • TANGAZO LA KAZI August 07, 2024
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2023 December 14, 2022
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2022 January 04, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kheri ya Siku ya Mazingira Duniani

    June 05, 2025
  • Utoaji wa dawa za minyoo na vitamin A kuanza Juni 1 Mbinga Mji

    May 31, 2025
  • MBINGA MJI YAFANYA TATHIMINI YA LISHE

    May 29, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA WAWASILI MBINGA MJI

    May 26, 2025
  • Tazama zote

Video

MAONYESHO YA NANENANE 2023 MBINGA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.