• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga Town Council
Mbinga Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA MBINGA ATEMBELEA MIRADI YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 1.765

Tarehe ya kuwekwa: September 27th, 2023



Na Alex Nelson Malanga


Afisa Habari---MTC


Mbinga.  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga (MTC) mwishoni mwa wiki (Septemba 23, 2023) alikagua miradi tisa yenye thamani ya shilingi bilioni 1.765 inayotekelezwa na Halmashauri hiyo.


Miradi hiyo pamoja na thamani yake kwenye mabano ni ujenzi wa shule ya sekondari katika kata ya Matarawe (Shilingi milioni 560.6), kituo cha afya cha Mbangamao (Shilingi milioni 500) na ujenzi wa shule ya Msingi Kipika katika kata ya Matarawe (Shilingi milioni 331.6).  


Miradi mingine ni ujenzi wa nyumba mbili za walimu katika shule ya sekondari Lusonga (Shilingi milioni 95), Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu matatu ya vyoo katika Shule ya Msingi Mbangamao (Shilingi milioni 53.1) na ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu matatu ya vyoo katika shule ya msingi Luhangai (Shilingi milioni 53.1).


Pia Mkurugenzi akiambatana na wakuu wa idara na vitengo alitembelea mradi wa Shule ya Msingi Makatani (Shilingi milioni 53.1) unaohusisha ujenzi wa madarasa mawili na matundu matatu ya vyoo, ujenzi wa madarasa mawili na matundu matatu ya vyoo katika Shule ya Msingi Tanga (Shilingi milioni 53.1)  pamoja na ujenzi wa madarasa  mawili ya elimu ya awali na matundu sita ya vyoo katika Shule ya Msingi Kiwanjani (Shilingi milioni 66.3).    


Imekuwa  ni utamaduni wa Mkurugenzi kuongozana na wasaidizi wake kwenda kwenye miradi ili kujua maendeleo ya utekelezaji hatua kwa hatua.    


Kwa lugha nyingine unaweza kusema kwa Halmashauri ya Mji wa Mbinga ni ‘Kazi iendelee’ kwa kasi na viwango vya hali ya juu.  


Akizungumza wakati wa ziara Bi. Amina aliwataka mafundi kuendelea kufanya kazi kwa kasi na ubora wa hali ya juu.


“Mama Samia (Rais wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan) anatupenda sana na ndio maana katuletea miradi kwa hiyo tusimuangushe,”alisema Bi. Amina.



Mhandisi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Bw. Peter Lupembe aliwahi kunukuliwa akisema mradi wa Sequip wa shule ya sekondari katika kata ya Matarawe  unahusisha ujenzi wa jengo la madarasa nane, maabara tatu, Maktaba, Jengo la Tehama, matundu kumi ya vyoo, kichomea taka na jengo la utawala.


Mradi huo ambao uko kwenye hatua ya msingi, pia unahusisha ujenzi wa jengo la Tehama, maktaba, matundu 10 ya vyoo na kichomea taka.



Kwa upande mwingine utekelezaji wa mradi wa kituo cha afya cha Mbangamao uko kwenye hatua ya mwisho ya utekekelezaji.


Mradi huu unahusisha ujenzi wa jengo la wazazi na chumba cha upasuaji, maabara, jengo la kufulia, wodi, njia za kuunganisha wodi moja na nyingine, jengo la wagonjwa wa nje (OPD) na ujenzi wa kichomea taka.



Wakati kwa upande wake mradi wa Shule ya Msingi Kipika unahusisha ujenzi wa madarasa 9, matundu 18 ya vyoo na jengo la utawala, mradi wa  Shule ya Msingi Mbangamao unahusisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu matatu ya vyoo.

Matangazo

  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA June 04, 2025
  • TANGAZO LA KAZI August 07, 2024
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2023 December 14, 2022
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2022 January 04, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kheri ya Siku ya Mazingira Duniani

    June 05, 2025
  • Utoaji wa dawa za minyoo na vitamin A kuanza Juni 1 Mbinga Mji

    May 31, 2025
  • MBINGA MJI YAFANYA TATHIMINI YA LISHE

    May 29, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA WAWASILI MBINGA MJI

    May 26, 2025
  • Tazama zote

Video

MAONYESHO YA NANENANE 2023 MBINGA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.