• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Government Web Framework

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Government Web Framework

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

MKUU WA MKOA AITAKA MBINGA MJI KUKUZA BIASHARA NA NCHI JIRANI

Tarehe ya kuwekwa: April 4th, 2024


Na Alex Nelson Malanga


Afisa Habari….Mbinga Mji


Mbinga. Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Kanali Ahmed Abbas Ahmed ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga kudumisha mahusiano ya kibiashara na nchi jirani za Msumbiji na Malawi.


Akizungumza mwishoni mwa wiki jana wakati wa kikao kazi na kamati ya fedha na timu ya wataalamu wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga kujadili taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya kamati ya kudumu ya bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Kanali Ahmed alisema wito huo ni agizo la Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.


Ikumbukwe kuwa Halmashauri ya Mji wa Mbinga inazalisha kwa wingi mazao ya biashara na chakula na hivyo fursa hiyo ikitumiwa vizuri itasaidia kukuza biashara na nchi jirani za Msumbiji na Malawi.


“Mheshimiwa Rais (Dkt Samia Suluhu Hassan) anatutaka tutengeneze mahusiano mazuri na jirani zetu ambao ni Msumbiji na Malawi ili kuongeza kasi ya ufanyaji biashara baina yetu,” alisema Mhe. Mkuu wa Mkoa.


Aliendelea kusema: “Ili tuongeze ujazo wa biashara na jirani zetu, Mhe. Rais ametuagiza tuendelee kuboresha mazingira ya biashara ili kuvutia wafanyabiashara na wawekezaji katika nchi yetu.”      


Mwaka 2022, kiwango cha biashara kati ya Tanzania na Msumbiji kilikuwa dola za Marekani milioni 81.8 (Sh209.8 bilioni), kwa mujibu wa OEC, tovuti mahususi kwa data za biashara za kimataifa.


Kati ya kiasi hicho, Tanzania ilipeleka Msumbiji bidhaa zenye thamani ya dola milioni 64.5 (Sh165.4 bilioni) na kupokea bidhaa za dola milioni 17.3 (Sh44.4 bilioni).


Wakati miongoni mwa bidhaa zinazouzwa Msumbiji kutoka Tanzania zikiwa ni mashuka, chupa za glasi, samaki, mahindi, maharage, waya za alumini, mbao na mawese, zile zinazoingizwa nchini ni  jenereta, bidhaa za urembo, mishumaa na utambi, miongoni mwa nyingine.


Kwa upande mwingine katika mwaka huo wa 2022, kiwango cha biashara kati ya Tanzania na Malawi kilikuwa dola za Marekani milioni 111.5 (Sh286 bilion).


Kati ya kiasi hicho, Tanzania ilipeleka Malawi bidhaa zenye thamani ya dola milioni 38.7 (Sh99.3 bilion) na kupokea bidhaa za dola milioni 72.8 (Sh186.7 bilion).


Wakati miongoni mwa bidhaa zinazouzwa Malawi zikiwa zile za kufanyia usafi, urembo, chupa za glasi na mazao ya chakula na biashara, Tanzania inauziwa karanga na soya, miongoni mwa bidhaa nyingine.  


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Mh. Kelvin Mapunda alisema: “kama Halmashauri tutafanya kila tuwezalo kutengeneza mazingira rafiki ya biashara ili kuongeza kiwango cha biashara na majirani zetu wa Malawi na Msumbiji.”


Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Bi. Amina Seif alisema: “Sisi kama wataalamu wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga tutahakikisha hatuwi kikwazo kwa wafanya biashara.”


Kumekuwa na wito wa mara kwa mara kwa nchi za Afrika kushirikiana katika kufanya biashara baina yao kwa kuwa nchi hizo zimekuwa zikifanya biashara zaidi na watu wa nje hususani nchi za Ulaya na Asia.


Licha ya kubarikiwa na rasilimali nyingi, takwimu zinaonesha kuwa kiwango cha biashara miongoni mwa nchi za Afrika ni asilimia 20 tuu ya biashara yote ambayo bara hilo la pili kwa ukubwa duniani linafanya na dunia.

Matangazo

  • KUITWA KATIKA USAHILI October 13, 2025
  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI May 25, 2022
  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA June 04, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 13, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kambi ya madaktari Bingwa wa Dkt Samia Suluhu Hassan yaendelea kutoa Huduma Halmashauri ya Mji Mbinga

    September 24, 2025
  • KISHINDO CHA MHE.RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN MBINGA MJI KATIKA MIRADI YA ELIMU

    August 29, 2025
  • KISHINDO CHA MHE.RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN MBINGA MJI KATIKA MIRADI YA ELIMU

    August 29, 2025
  • KISHINDO CHA MHE.RAIS,DKT. SAMIA SULUHU HASSAN MBINGA MJI KATIKA MIRADI YA ELIMU

    August 29, 2025
  • Tazama zote

Video

MAONYESHO YA NANENANE 2023 MBINGA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Government Web Framework

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki