• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Government Web Framework

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Government Web Framework

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

MKUU WA WILAYA YA MBINGA AZINDUA KAMPENI YA USAFI IJULIKANAYO KAMA MANGOSONGO OPARESHENI SAFISHA MJI: MBINGA ING'AE

Tarehe ya kuwekwa: September 4th, 2023



Na Alex Nelson Malanga


Afisa Habari- MTC


Mbinga. Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Aziza Mangosongo leo Septemba 4, 2023 amezindua kampeni ya usafi ya wiki moja yenye lengo la kuifanya Mbinga kuwa safi na yenye mvuto zaidi machoni pa watu.


Uzinduzi wa kampeni itakayotamatishwa Septemba 10, ulifanywa katika maeneo ya Soko la Mtumba, Soko Kuu, Stendi kuu, Manzese, Machinjio na Viunga vya bustani vilivyopo barabara kuu ya Songea- Mbamba Bay.


Kama unadhani kampeni hii inayokwenda kwa jina la ‘Mangosongo Oparesheni Safisha Mji: Mbinga ing’ae’, itaishia kwenye maeneo hayo, unakosea sana.


Kampeni iliyobuniwa na Mhe. Mkuu wa Wilaya itagusa kata zote za Wilaya ya Mbinga na viunga vyake na pia zoezi la usafi litakuwa endelevu.


Akizindua kampeni hiyo Mhe. Aziza aliwataka watendaji wa kata na mitaa kufanya kazi kwa bidii bila kusukumwa.


Pamoja na Mhe. Mkuu wa Wilaya, viongozi wengine waliohudhuria ufunguzi wa kampeni hiyo kabambe ya usafi ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbinga Bi. Pendo Ndumbaro, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga (MTC) Mhe. Kelvin Mapunda na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi. Amina Seif.


 Wengine ni maafisa Afya wa Wilaya, baadhi ya wakuu wa idara wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga na Maafisa watendaji wa kata na vijiji.  


Mhe. Aziza alionesha kukerwa na kulegalega kwa kampeni ya usafi ya kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi.


“Hii haikubaliki. Tunataka Mbinga ambayo ni safi,” alisema Mhe. Aziza.


 Aliongeza kwa kusema: “Watendaji wa Kata na Mitaa lazima muache ‘legacy’(alama) na legacy huwa haijifichi.”


“Lazima mjiulize siku ukihama kutoka mtaa au kata moja kwenda nyingine utakumbukwa kwa lipi?


Alisema kwa viongozi hao kupata mafanikio makubwa na hivyo kuacha alama kwa vizazi vijavyo, wanapaswa kuandaa mpango kazi na kuhakikisha wanaufanyia kazi.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Mhe. Mapunda alimshukuru Mkuu wa Wilaya kwa mawazo yake mazuri ya kusaidia Halmashauri.


Alieleza haja ya kuifanya Mbinga kuwa kioo cha jamii linapokuja suala la usafi.


“Watendaji lazima tutekeleze yale tunayoelekezwa na Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya,” alisema Mhe. Mapunda.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Bi. Amina, kwa upande wake, aliwataka watendaji wa Mitaa na Kata kusimamia kikamilifu zoezi la usafi kwenye maeneo yao.


“Usafi unaofanyika wiki hii tunataka uwe endelevu kwani tunataka Mbinga yetu ing’ae ,” alisema Bi. Amina huku akimshukuru Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya kwa kuja na kampeni hii murua.    


Kwa upande wake Afisa Afya wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Bw. Felix Matembo alisema atafanya kila liwezekanalo kuhakikisha Mji wa Mbinga unang’aa.


Alisema ili kufanikisha ndoto ya kuwa na Mbinga itakayomfanya mtu asichoke kuitazama, atafanya kazi kwa kushirikiana na watendaji wa mitaa na kata.  


“Kampeni hii itachochea ufanisi katika usafi wa mazingira,” alisema Bw. Matembo.


Ikiwa ni ishara ya kuyafanya mazingira kuwa na mvuto zaidi siku za usoni, zoezi la usafi siku ya kwanza ya kampeni lilienda sambamba na upandaji miti katika viunga vya bustani vilivyopo barabara kuu ya Songea- Mbamba Bay.


Mhe. Mkuu wa Wilaya, Katibu Tawala wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga waliungana na wadau wengine wa mazingira katika zoezi la upandaji miti.  












Matangazo

  • KUITWA KATIKA USAHILI October 13, 2025
  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI May 25, 2022
  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA June 04, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 13, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kambi ya madaktari Bingwa wa Dkt Samia Suluhu Hassan yaendelea kutoa Huduma Halmashauri ya Mji Mbinga

    September 24, 2025
  • KISHINDO CHA MHE.RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN MBINGA MJI KATIKA MIRADI YA ELIMU

    August 29, 2025
  • KISHINDO CHA MHE.RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN MBINGA MJI KATIKA MIRADI YA ELIMU

    August 29, 2025
  • KISHINDO CHA MHE.RAIS,DKT. SAMIA SULUHU HASSAN MBINGA MJI KATIKA MIRADI YA ELIMU

    August 29, 2025
  • Tazama zote

Video

MAONYESHO YA NANENANE 2023 MBINGA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Government Web Framework

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki