• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga Town Council
Mbinga Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

MRADI WA SHULE YA MSINGI MATENGO ‘KIPIKA’ WAZIKOSHA KAMATI ZA FEDHA NA ELIMU

Tarehe ya kuwekwa: January 25th, 2024


Na Alex Nelson Malanga


Afisa Habari…Mbinga TC


Mbinga. Wajumbe wa Kamati za Fedha na Elimu kutoka Halmashauri ya Mji wa Mbinga siku ya Jumanne, Januari 23, 2024 walitembelea miradi mitano yenye thamani ya Shilingi bilioni 1.1 inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo.


Wajumbe hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Mhe. Kelvin Mapunda walionekana kukoshwa na ubora wa miradi hiyo huku mradi wa shule ya Msingi Matengo almaarufu Kipika ukionekana kukonga zaidi nyoyo za wajumbe hao.  


Nyuso zao zikiwa zimefunikwa na tabasamu pana, wajumbe wa kamati waliumwagia sifa kemkem mradi wa Matengo ‘Kipika’ uliogharimu kiasi cha Shilingi milioni 331.6 huku wakisema una mvuto wa aina yake.


Shule ya Msingi Matengo yenye madarasa tisa, matundu 16 ya vyoo na jengo la utawala, ilifunguliwa rasmi Januari 8, 2024 na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Aziza Mangosongo.


Wajumbe wa kamati pia walivutiwa na ubora wa miradi mingine pamoja na gharama zake kwenye mabano; Shule ya Sekondari Dkt. Philip Mpango (Shilingi milioni 560.6) iliyofunguliwa Januari 8, 2024 na ujenzi wa nyumba ya walimu wawili wa shule ya sekondari Lusonga (Shilingi milioni 95).


Kamati hizo mbili pia zilitembelea miradi ya Shule ya Msingi Kiwanjani (Shilingi milioni 66.3) na Shule ya Msingi Tanga (Shilingi milioni 53.1).


Sura yake ikiwa inajieleza kila kitu, Diwani wa Kata ya Mateka Mhe. Method Ndunguru alisema mradi wa Kipika ni wa mfano na kwamba hutoa fursa kwa wengine kuiga.


Huku akielekeza macho yake kwa Diwani wa Kata ya Matarawe Mhe. Kelvin Mapunda, Mhe. Ndunguru alisema: “Shule yako ni shule ya mfano. Inatoa Taswira ya hapa Mjini.”


Diwani wa Kata ya Lusonga Mhe. Magreth Ngongi aliusifia mradi wa Kipika huku akimpongeza diwani wa kata hiyo Mhe. Mapunda kwa usimamizi uliotukuka.


“Muonekano wa shule hii unamvutia kila mzazi kumleta mwanaye,” alisema Mhe. Magreth.


Diwani wa Kata ya Luhuwiko Mhe. David Mapunda alisema: “nimeridhishwa na ubora wa majengo.”


Mwenyekiti wa Halmashauri, kwa upande wake, alimshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Halmashauri fedha kwaajili ya miradi ya maendeleo.


“Rais wetu anawajali wananchi na ndio maana anafanya kila awezalo kusogeza huduma za kijamii karibu yao,” alisema Mhe. Mapunda.


Kwa upande mwingine, Mhe. Mapunda alimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Bi. Amina Seif kwa kazi nzuri ya kusimamia miradi ya maendeleo.

Matangazo

  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA June 04, 2025
  • TANGAZO LA KAZI August 07, 2024
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2023 December 14, 2022
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2022 January 04, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kheri ya Siku ya Mazingira Duniani

    June 05, 2025
  • Utoaji wa dawa za minyoo na vitamin A kuanza Juni 1 Mbinga Mji

    May 31, 2025
  • MBINGA MJI YAFANYA TATHIMINI YA LISHE

    May 29, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA WAWASILI MBINGA MJI

    May 26, 2025
  • Tazama zote

Video

MAONYESHO YA NANENANE 2023 MBINGA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.