Miradi mine yenye thamani ya Tsh milioni 681.9 imezinduliwa na mmoja kuwekwa jiwe la msingi na Mwenge wa uhuru 2022, katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga Mkoani Ruvuma. Akifungua kiwanda cha kusindika unga cha AMNEC SUPER SEMBE kilichopo kata ya Utiri Halmashauri ya Mji wa Mbinga, kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa 2022 Ndg Sahili Nyanzabara Geraruma amempongeza mwekezaji wa kiwanda hicho Ndg Julius Mashauri kwa uthubutu wake wa kuweza kutoa ajira kwa vijana na kutoa rai kwa wafanya biashara kuendelea kuwekeza ili kutoa ajira zaidi katika Halmashauri hiyo.
Aidha Ndg Geraruma amemshukuru kiongozi wa dini wa jimbo katoliki la mbinga Mhasham Baba Askofu John Ndimbo kwa ujenzi wa jingo la OPD kwaajili ya upanuzi wa huduma ya afya, ikiwa nisehemu ya ujezi wa mradi wa kituo cha afya cha Mtakatifu Gabriel na kumuomba kuzingatia garama za matibabu zenye unafuu kwa wanachi. Sambamba na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo hicho cha Afya, pia kiongozi huyo wa Mwenge kitaifa 2022 alishiriki zoezi la kugawa vyandarua vilivyo andaliwa na kituo hicho na kusisitiza wakavitumie vyema, ikiwa nisehemu ya kaulimbiu ya Mwenge ya kudumu isemayo “Ziro malaria inaanza na mimi nachukua hatutua kuitokomeza”.
“Sensa ni msingi wa mipango ya maendeleo; shiriki kuhesabiwa, tuyafikie Maendeleo ya Taifa”. Nikaulimbiu ya mwenge wa uhuru 2022 ambapo zoezi la uwekaji Amwani ya makazi na postikodi ilimekuwa likiendelea, hivyo kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge kitaifa katika uzinduzi wa zoezi hilo akapatanafasi na kutoa rai kwa wananchi kujitokeza katika Sensa ya watu na makazi, itakayo fanyika Agosti 22 2022. Miradi mingine iliyo funguliwa ni pamoja na TCRP 5441 (UVIKO-19) ambapo Shule ya sekondari Luhuwiko moja kati ya shule ambayo ikiwakilisha, kwa kufunguliwa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, vilivyo ghalimu Tsh Milioni 40. Aitha mradi mwingine ni Klabu ya wapinga Rushwa Wanafunzi wa chuo cha Maendeleo Mbinga FDC.
Sambamba na hayo, kiongozi huyo wa Mwenge amewakumbusha vijana kuunda vikundi vya ujasiliamali ili kuendelea kupata mikopo isiyo na riba kutoka Halmashauri inayo tokana na asilimia kumi ili kujiimarisha uchumi na kuleta maendeleo kwa Taifa. Hayo ameyasema marabaada ya kutembelea kikundi cha vijana Tujikwamue kwalengo la kukabidhi pikipiki kwa kikundi hicho na kubaini baadhi ya mapungufu ivyo kushauri vijana hao wapewe mafunzo ya kutosha ya uendeshaji ili waweze kuwa mahili katika biashara ya usafirishaji, maarufu kama bodaboda.
Na Makangury
MBINGA
Sanduku la Barua: P.O.BOX 135
Simu ya Mezani: +225 - 2640664
Mobile: +225 – 2640664
Barua pepe: td@mbingatc.go.tz
Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.