• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Government Web Framework

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Government Web Framework

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

NIDA YAFIKIA ASILIMIA 83.2 YA LENGO LA USAJILI MBINGA

Tarehe ya kuwekwa: December 23rd, 2023


Na Alex Nelson Malanga


Afisa Habari---MTC


Mbinga. Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Wilaya ya Mbinga imefikia asilimia 83.2 ya malengo ya usajili wa watu 223,657.


Hayo yalisemwa siku ya Alhamis ya Disemba 21, 2023 wakati wa Uzinduzi wa zoezi la siku 14 la Ugawaji Vitambulisho vya Taifa kwa Wilaya ya Mbinga, katika tukio ambalo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Bi. Aziza Mangosongo.


Akizungumza wakati wa uzinduzi, Afisa Usajili Mwandamizi wa NIDA Bw. Ibrahim Liduke alisema hadi Novemba 30, 2023 idadi ya watu waliosajiliwa ilikuwa 185,986.


“Hii ni sawa na asilimia 83.2 ya lengo la kusajili watu 223,657,” alisema Bw.Liduke.


Alisema kwa sasa watagawa vitambulisho vya Taifa 131,181 ambavyo vimezalishwa hivi karibuni kwa Wananchi na Wakazi wa Wilaya ya Mbinga.


Hii itapelekea kufikisha idadi ya Wananchi 164,275 watakaokuwa na vitambulisho vya Taifa sawa na asilimia 88.3 ya wananchi wote waliojiandikisha, kwa mujibu wa Bw. Liduke.


Zoezi hili la ugawaji wa vitambulisho litafanyika kwa utaratibu wa kuvisambaza hadi ngazi ya kata na kukabidhiwa Mtendaji Kata kabla ya kuvikabidhi kwa watendaji wa Mitaa na Vijiji ambao ndio watakuwa na jukumu la kuvigawa kwa wananchi.


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Mhe. Aziza aliwataka watendaji kata wawahamasishe wananchi kujitokeza kwa wingi kufuata vitambulisho vyao.


“Ugawaji wa vitambulisho utakata kiu ya muda mrefu ya wananchi wa Wilaya ya Mbinga waliokuwa wakisubiri vitambulisho vyao kwa muda mrefu,” alisema Mhe. Aziza.


Mbunge wa Mbinga Mjini Mhe. Jonas Mbunda alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweka sera nzuri kuhakikisha kila mwananchi anapata kitambulisho.


“Tunamshukuru Mhe. Rais kwa kutoa zaidi ya bilioni 42 kwaajili ya uzalishaji wa vitambulisho vya Taifa (Milioni 13),” alisema Mh. Mbunda.


Wengine waliohudhuria katika tukio la uzinduzi ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Bi. Amina Seif na wakuu wa Idara na vitengo.

Matangazo

  • KUITWA KATIKA USAHILI October 13, 2025
  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI May 25, 2022
  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA June 04, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 13, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kambi ya madaktari Bingwa wa Dkt Samia Suluhu Hassan yaendelea kutoa Huduma Halmashauri ya Mji Mbinga

    September 24, 2025
  • KISHINDO CHA MHE.RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN MBINGA MJI KATIKA MIRADI YA ELIMU

    August 29, 2025
  • KISHINDO CHA MHE.RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN MBINGA MJI KATIKA MIRADI YA ELIMU

    August 29, 2025
  • KISHINDO CHA MHE.RAIS,DKT. SAMIA SULUHU HASSAN MBINGA MJI KATIKA MIRADI YA ELIMU

    August 29, 2025
  • Tazama zote

Video

MAONYESHO YA NANENANE 2023 MBINGA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Government Web Framework

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki