Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga wamepongezwa kwa kuweza kutenga na kutoa fedha kwa asiliamia miamoja kwa makaundi maalaum Wanawake Vijana na Watu wenye ulemavu. Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe; Brig. Balozi Wilbert Ibuge wakati wa kikao cha baraza maalumu la kupitia na kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga. Sambamba na hayo Mkuu huyo wa Mkoa ameendelea Kuipongeza Halmashauri hiyo kwa kuvuka lengo la makusanyo ya Mapato ya ndani, kufikia asilimia miamoja na tisa, awali Halmashauri hiyo ilikadiria kukusanya kiasi cha Tsh Billion 1,787,202,000 na wamekusanya Tshs Bilion 1,953,688,334 sawa na asilimia 109.
Mkuu huyo wa Mkoa ameendelea kuipongeza Halmashauri hiyo kwa kuendelea kupata Hati safi kwa miaka mitano mfululizo na kusema hii ni ishara nzuri kiutendaji na usimamizi mzuri wa mapato na matumizi ya fedha za Serikali. Sambamba na kupata Hati safi Balozi Ibuge amesisitiza usimamizi wenye ueledi na kuahakikisha watendaji wanazuia hoja kwa kufuata miongozo, sheria na kanuni za matumizi ya fedha za umma. Hata hivyo ameongeza na kusisitiza kuendelea kufuta hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali na kuzimaliza ifikapo mwezi wa tisa.
Kwa Upande wake Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe: David Mapunda amemshukuru Mkuu huyo wa Mkoa na kuhaidi kuyatekeleza maelekezo aliyoyatoa akishirikiana madiwani na wataalamu wa Halmashauri hiyo. Hata hivyo Mhe: David amesisitiza kwa madiwani kuendelea kusimamia ukusanyaji wa mapato ili kuendelea kufanya vizuri zaidi katika eneo hilo.
Na Makangury
MBINGA
Sanduku la Barua: P.O.BOX 135
Simu ya Mezani: +225 - 2640664
Mobile: +225 – 2640664
Barua pepe: td@mbingatc.go.tz
Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.