• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga Town Council
Mbinga Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

TIMU YA BODABODA YATWAA UBINGWA BONANZA LA USAFI WA MAZINGIRA KWA KUWAGARAGAZA MALAIKA UVIKAMBI

Tarehe ya kuwekwa: September 11th, 2023



Na Alex Nelson Malanga


Afisa Habari----MTC


Mbinga:  Kilele cha kampeni ya usafi ijulikanayo kama Mangosongo Oparesheni Safisha Mji: Mbinga ing’ae, jana Septemba 10, 2023 kilipambwa na fainali ya bonanza la usafi wa mazingira ambapo timu za Bodaboda FC na Malaika Uvikambi FC zilimenyana vikali.


Katika mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Sekondari Makita uliopo katika kata ya Masumuni timu ya Bodaboda iliibuka kidedea kwa ushindi wa magoli mawili kwa nunge mbele ya mgeni rasmi, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Aziza Mangosongo,


Ilikuwa dakika ya 49 ya kipindi cha pili cha mchezo ambapo Innocent Nchimbi, mchezaji namba mbili akiwa amevalia jezi namba tatu mgongoni, aliwanyanyua mashabiki wa Bodaboda vitini mara baada ya kufunga goli murua.


Kama hiyo haitoshi dakika tatu baadaye mchezaji namba nane, Emmanuel Shao alipigilia msumari wa pili na wa mwisho na hivyo kuwawezesha Bodaboda kutoka kifua mbele kwa ushindi wa magoli mawili kwa sinia.


Mchezo huo ulioanza majira ya saa 11.05 jioni ukitanguliwa na ngoma za asili kutoka vikundi mbalimbali, sarakasi, mashairi kutoka shule ya Sekondari Mbinga, mchezo wa kuvuta kamba, maigizo na kareti, ulikuwa ni wa vuta nikute, piga nikupige, niachie nikuachie, vuta shati langu nami nivute lako.


Mchezo huo wa fainali, uliochezeshwa na Gelmanus Mwambela kama mwamuzi wa kati na kusaidiwa na Jesca Mipunga na John Komba, ulikuwa ni kivumbi na jasho kwani kila timu ilitaka kuibuka kifua mbele.


Wakati timu ya bodaboda ikitinga fainali kwa kuichabanga Mtumbani FC kwa mikwaju ya penati 7 kwa sita katika hatua ya nusu fainali siku ya Jumamosi Septemba 9, 2023, timu ya Malaika Uvikambi ilifika hatua hiyo kwa kuigaragaza Lusonga.


Wakati mshindi wa fainali akienda nyumbani na shilingi laki moja, mbuzi mmoja na mpira, mshindi wa pili alijinyakulia Shilingi 50,000 na kuku wawili.


Pamoja na Mkuu wa Wilaya, bonanza hilo lilihudhuriwa na viongozi wengine ambao ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbinga Bi. Pendo Daniel na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga (MTC) Bi. Amina Seif, ambaye baadaye alipatwa na dharura na hivyo kukaimisha  nafasi hiyo kwa Dkt Kung’e Nyamuryekung’e.


Wengine waliohudhuria ni madiwani wa Kata mbalimbali, wakuu wa idara kutoka ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Halmashauri ya Mji wa Mbinga pamoja na watendaji wa Kata na Mitaa.


Akizungumza baada ya mchezo wa fainali uliohudhuriwa na mamia ya wakazi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga, Mhe. Mangosongo aliipongeza timu ya Bodaboda FC kwa kuwafanya Malaika Uvikambi waangukie pua.


“Hongereni kwa kuibuka kuwa wababe wa mashindano haya. Mmecheza vizuri, mnastahili ushindi,” alisema Mhe. Mangosongo.


Akizungumza kabla ya kwenda kwenye majukumu mengine, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Bi. Amina aliahidi kushirikiana na wasaidizi wake kuendelea kusimamia zoezi la usafi katika eneo lake la utawala.


Kwa upande wake Dr Nyamuryekung’e alisema: “Tutasimamia kikamilifu zoezi la usafi kwenye halmashauri yetu ili iendelee kung’aa.”


 Naye Afisa Afya wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Bw. Felix Matembo alimwambia mkuu wa Wilaya: “Tutaendelea na zoezi hili la usafi kwasababu jukumu letu ni kukuunga mkono.”


Mhe. Aziza Septemba 4, 2023 alizindua kampeni ya usafi ya wiki moja yenye lengo la kuifanya Mbinga kuwa safi na yenye mvuto zaidi machoni pa watu.


Uzinduzi wa kampeni ulifanywa katika maeneo ya Soko la Mtumba, Soko Kuu, Stendi kuu, Manzese, Machinjio na Viunga vya bustani vilivyopo barabara kuu ya Songea- Mbamba Bay, kabla ya baadae kuendelea katika maeneo mengine.

Matangazo

  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA June 04, 2025
  • TANGAZO LA KAZI August 07, 2024
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2023 December 14, 2022
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2022 January 04, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kheri ya Siku ya Mazingira Duniani

    June 05, 2025
  • Utoaji wa dawa za minyoo na vitamin A kuanza Juni 1 Mbinga Mji

    May 31, 2025
  • MBINGA MJI YAFANYA TATHIMINI YA LISHE

    May 29, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA WAWASILI MBINGA MJI

    May 26, 2025
  • Tazama zote

Video

MAONYESHO YA NANENANE 2023 MBINGA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.