• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Government Web Framework

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Government Web Framework

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

UZALISHAJI WA MAZAO YA CHAKULA NA BIASHARA WAONGEZEKA KWA ASILIMIA 7.9

Tarehe ya kuwekwa: October 24th, 2023


Na Erasto George


Mbinga. Uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga (MTC) uliongezeka kwa asilimia 7.9 katika msimu wa 2022/23 ikilinganishwa na mwaka wa nyuma yake.


Siku ya Oktoba 24, 2023 Afisa Kilimo na Msimamizi wa Pembejeo wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Bw. Andrew Chiwinga alisema ongezeko la uzalishaji lilitokana na mfumo mzuri wa upatikanaji wa mbolea za ruzuku.


Bw. Chiwinga alisema kuwa katika msimu wa 2022/23 uzalishaji uliongeza kufikia tani 80,900 ikilinganishwa na tani 75,000 zilizozalishwa mwaka 2021/22.



"Mfumo wa mbolea za ruzuku umewasaidia wakulima kupata mbolea kwa bei nafuu na kwa wakati na hivyo kuongeza tija katika kilimo,” alisisitiza.



Bw.Chiwinga alisema kwa msimu uliopita walipokea mbolea tani 15,613 ikilinganishwa na matarajio ya tani 10,500.



Aidha, aliongeza kuwa ongezeko hilo lilitokana na wilaya nyingine za Mbinga vijijini na Nyasa kuchukua mbolea kutoka Mbinga Mji.



Pia Bw. Chiwinga alisema kwa Halmashauri ya Mji wa  Mbinga, mahitaji yao  ya mbolea yanakadiriwa kuwa tani 12,500 kwa mwaka 2023/24 ikilinganishwa na tani 10,500.  


Hii, alieleza, inatokana na kuongezeka kwa wakulima wanaojisajili katika mfumo wa mbolea ya ruzuku.


Bw. Chiwinga alisema msimu uliopita waliweza kuwasajili na kuwaingiza kwenye mfumo wakulima 21,099  na kuwapatia namba za kununulia mbolea ya ruzuku.



Ili msimu huu wa 2023/24 wakulima wengi zaidi wanufaike na mbolea ya ruzuku aliwataka kwenda katika maeneo waliojiandikisha kuhakiki taarifa zao.



Bw. Chiwinga alisema mbali  na uhakiki wa taarifa, pia usajili mpya kwa wale ambao hawakujiandikisha msimu uliopita unaendelea katika kata na vijiji vya Halmashauri ya Mji wa Mbinga.



Mkulima katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga Bw. Alex Saligo alisema hivi sasa  mbolea za ruzuku zinawasaidia sana wakulima tofauti na zamani ambapo kila muuzaji alikuwa anapanga bei yake.


Mkulima mwingine Bw. Erick Komba alisema baada ya serikali kuanza kutoa mbolea za ruzuku wameondokana na usumbufu kwa kuwa zinauzwa kwa bei elekezi.

Matangazo

  • KUITWA KATIKA USAHILI October 13, 2025
  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI May 25, 2022
  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA June 04, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 13, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kambi ya madaktari Bingwa wa Dkt Samia Suluhu Hassan yaendelea kutoa Huduma Halmashauri ya Mji Mbinga

    September 24, 2025
  • KISHINDO CHA MHE.RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN MBINGA MJI KATIKA MIRADI YA ELIMU

    August 29, 2025
  • KISHINDO CHA MHE.RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN MBINGA MJI KATIKA MIRADI YA ELIMU

    August 29, 2025
  • KISHINDO CHA MHE.RAIS,DKT. SAMIA SULUHU HASSAN MBINGA MJI KATIKA MIRADI YA ELIMU

    August 29, 2025
  • Tazama zote

Video

MAONYESHO YA NANENANE 2023 MBINGA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Government Web Framework

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki