• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga Town Council
Mbinga Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

VYAMA VYA USHIRIKA MBINGA MJI KULIPA ASILIMIA 3 YA BEI KWA KILA KILO MOJA YA KAHAWA

Tarehe ya kuwekwa: October 17th, 2023



Na Rahma Mwaka & Elizabeth Newa


Mbinga. Vyama vya  Ushirika  wa Kilimo na Masoko ya kahawa (AMCOS) katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga vimekubaliana kulipa ushuru wa asilimia 3 ya bei kwa kila kilo moja ya kahawa kwa kuzingatia bei ya mnada wa siku husika.


Makubaliano hayo yalifikiwa katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano  wa Oddo Mwisho jana Oktoba 16, 2023 na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka vyama vyote vya ushirika vilivyopo katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga.


Mkuu wa idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Bw. Enock Ndunguru alisema msimu uliopita wakulima walikuwa wakilipa ushuru wa shilingi 150 kwa kilo ya kahawa bila kujali kiwango cha bei ambacho mkulima amekitumia katika mauzo yake.



"Kwa sasa mbali na asilimia 3, wakulima huchangia shilingi 20 kwa kila kilo moja ya kahawa, kiasi ambacho huelekezwa katika shughuli za maendeleo katika jamii," alieleza Bw. Ndunguru.



Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Mhe. Alex Andoya aliwapongeza wakulima wa kahawa kwa kuwa wana thamani kubwa katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga.



Alisisitiza haja ya kujenga mahusiano mazuri kati ya Halmashauri na wakulima ili kuisaidia serikali kupata mapato kupitia kahawa.


"Wataalamu hakikisheni mnawasaidia wakulima kuilinda kahawa ambayo inapatikana katika Halmashauri," aliagiza Mhe. Andoya.



Afisa Mapato wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Denis Muli alisema kahawa imekuwa na mchango mkubwa katika mapato ya Halmashauri.



Bw. Muli aliwataka viongozi wa AMCOS zote kuhakikisha wanalipia na kupata leseni za biashara na maghala ili kuepuka faini zinazoweza kujitokeza kama hawajafanya hivyo.



Mkuu wa idara ya Ardhi Bw. John Rikanga alivishauri vyama vya Ushirika wa Kilimo na Masoko  ya kahawa (AMCOS ) kuhakikisha vipande vya ardhi walivyonavyo vinapimwa na kuvimiliki kisheria.



Bw. Rikanga alisema kwa kufanya hivyo wataepuka migogoro ya mipaka, wataweza  kupandisha thamani ya ardhi waliyonayo na  kupitia nyaraka za umiliki wa ardhi zitawawezesha kukopa katika taasisi mbalimbali za kifedha.

Matangazo

  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA June 04, 2025
  • TANGAZO LA KAZI August 07, 2024
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2023 December 14, 2022
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2022 January 04, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kheri ya Siku ya Mazingira Duniani

    June 05, 2025
  • Utoaji wa dawa za minyoo na vitamin A kuanza Juni 1 Mbinga Mji

    May 31, 2025
  • MBINGA MJI YAFANYA TATHIMINI YA LISHE

    May 29, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA WAWASILI MBINGA MJI

    May 26, 2025
  • Tazama zote

Video

MAONYESHO YA NANENANE 2023 MBINGA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.