• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga Town Council
Mbinga Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

WAKAZI WA MBINGA WATAKIWA KUWA WAZALENDO

Tarehe ya kuwekwa: December 12th, 2023



Na Alex Nelson Malanga


Afisa Habari----MTC


Mbinga.  Viongozi mbalimbali kutoka Wilaya ya Mbinga wamewataka wakazi wa wilaya hiyo kuwa wazalendo kwa maslahi mapana ya Taifa la Tanzania.


Wito huo ulitolewa wakati wa kilele cha maadhimisho ya sherehe za miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika Jumamosi ya Disemba 9, 2023 katika Ukumbi wa Mkapa uliopo katika Shule ya Sekondari Kigonsera, Wilayani Mbinga.


Akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mbinga katika sherehe hizo, Kaimu Afisa Tawala wa Wilaya Bw. Karim Mzee alisema kila mkazi wa Mbinga anapaswa kuwa mzalendo kwa Taifa la Tanzania.


“ Tukifanya hivyo Tanzania itapiga hatua kubwa ya maendeleo kwa kuwa kila mmoja wetu atakuwa mlinzi wa Taifa letu,” alisema Bw. Mzee wakati wa maadhimisho yaliyobeba kauli mbiu: Umoja na Mshikamano ni chachu ya maendeleo ya Taifa letu.



Aliongeza: “Sisi hatuna ‘option’ (chaguo), Tanzania ndio mama, Tanzania ndio baba. Hatuna pengine pakwenda…kwa muktadha huo, lazima tuilinde na kutetea nchi yetu.”


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Mhe. Kelvin Mapunda alisema suala la uzalendo linapaswa kwenda sanjari na kuwa na kizazi cha vijana wasomi.


 Alisema ili taifa liwe na vijana wenye tija kwa maendeleo, wanafunzi wa shule ya Sekondari Kigonsera hawanabudi kusoma kwa bidii.


“Msimuache elimu aende zake. Someni kwa bidii ili mfaidike na dunia ijayo,” Mhe. Mapunda aliwaasa.  



Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Bi. Amina Seif aliwataka vijana kuwa wazalendo kwa manufaa mapana ya Taifa.


“Vijana wa Tanzania mnapaswa kushikamana, kuwa wazalendo na wasikivu. Lazima muwe vijana bora kwa Taifa,” alisisitiza Bi. Amina.



Kamanda wa Takukuru Wilaya ya Mbinga Frederick Msae aliwataka wakazi wa wilaya hiyo kujitolea maisha yao kwaajili ya Taifa la Tanzania.


“Ni vizuri tukawa wazalendo. Ni vizuri tukajitolea linapokuja suala la ujenzi wa Taifa letu,” alisema  Kamanda Msae.


Aliongeza: “Katiba inatutaka, na si kutuomba, kuwa wazalendo. Kwahiyo yeyote ambaye siyo mzalendo kimsingi anavunja katiba yetu.”


Alikemea wanaotumia mali za umma kwa manufaa binafsi na kusema kuwa huo sio uzalendo.


“Tusiwafumbie macho watumishi wa umma wanaojihusisha na vitendo vya ubadhilifu wa mali za umma ikiwa ni pamoja na vitendo vya rushwa,” Bw. Msae alitoa rai.


Maadhimisho ya sherehe za miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara yalianza tangu Disemba 1 mwaka huu kwa kufanya shughuli mbalimbali za jamii ikiwemo kupanda miti na kufanya usafi.


Kuanzia tar 1 mkuu wa Wilaya ya Mbinga Bi. Aziza Mangosongo alifanya matukio mbalimbali ikiwemo kugawa madawati  kwa shule, kupanda miti na kuongea na waandishi wa habari kuelezea namna Mbinga ilivyopiga hatua.


Pia alipata fursa ya kuongea na wakuu wa Wilaya ya Kyela na Wanging’ombe  kuelezea fursa zilizopo Wilaya ya Mbinga ili waone namna ya kuja kuwekeza huku.


Naye Mhe. Mapunda, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga alishiriki katika zoezi la upandaji miti maeneo mbalimbali ikiwemo katika shule mpya ya Sekondari Matarawe.


Tamati ya Maadhimisho ya sherehe za uhuru ilikuwa Disemba 9  ambapo ulifanyika mdahalo wa kujadili maendeleo endelevu ambayo Wilaya ya Mbinga imefikia kwa kipindi cha miaka 62.

Matangazo

  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA June 04, 2025
  • TANGAZO LA KAZI August 07, 2024
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2023 December 14, 2022
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2022 January 04, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kheri ya Siku ya Mazingira Duniani

    June 05, 2025
  • Utoaji wa dawa za minyoo na vitamin A kuanza Juni 1 Mbinga Mji

    May 31, 2025
  • MBINGA MJI YAFANYA TATHIMINI YA LISHE

    May 29, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA WAWASILI MBINGA MJI

    May 26, 2025
  • Tazama zote

Video

MAONYESHO YA NANENANE 2023 MBINGA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.