• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga Town Council
Mbinga Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

WANANCHI WAKUMBUSHWA KUWATHAMINI WAZEE.

Tarehe ya kuwekwa: October 6th, 2023


Na Elizabeth Newa, Rahma Mwaka & Erasto George


Mbinga.  Kaimu Afisa Tawala wa Wilaya ya Mbinga Bw. Andrea Mhagama, aliitumia siku ya wazee duniani kuikumbusha jamii juu ya umuhimu wa kuwathamini, kuwajali na kuwatunza wazee dhidi ya vitendo vya ukatili.


Bw. Mhagama alikuwa mgeni rasmi wa maadhimisho yaliyofanyika Oktoba 1, 2023, katika viwanja vya ofisi ya Kata ya Luhuwiko.


“Jukumu la kuwatunza wazee ni la jamii nzima kwa kuwa enzi za ujana wao nguvu zao zilitumika kuzalisha mali na kuliendeleza Taifa,” alisema Bw. Mhagama.


Alisistiza: "Maendeleo haya tunayoyaona sasa ni msingi mzuri uliowekwa na wazee hivyo ni jukumu letu sote kuwatengenezea mazingira mazuri ili waendelee kufurahia uzee wao.”


Bw. Mhagama ambaye  alimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Aziza Mangosongo aliongeza kuwa kauli mbiu ya siku hiyo:  "Uthabiti wa Wazee kwenye Dunia yenye Mabadiliko" inalenga kuelimisha jamii juu ya mchango wa wazee kwenye Dunia ambayo ina mabadiliko makubwa ya sayansi na teknolojia.


Pia alìsema wazee wakiishi bila kubaguliwa, kunyanyaswa na kufanyiwa vitendo vya ukatili wana uwezo wa kuendelea kufanya kazi na kuwashauri vijana kuhusu umuhimu wa kufanya kazi na kuchochea maendeleo ya Taifa.

Aliwaagiza wataalamu wa afya kuhakikisha kuna sehemu ya kuwahudumia wazee ili wasipate changamoto kama ilivyoagizwa na serikali na kutoa ufafanuzi mzuri ili wazee waelewe vizuri  mwenendo wa afya zao.

Afisa Maendeleo ya jamii wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Bi. Cecilia Mbata aliyemuwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Bi Amina Seif, alisema wanajitahidi kutoa huduma mbalimbali kwa wazee kwa kuzingatia miongozo na maelekezo.

"Kupitia kitengo cha TASAF (Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini) na idara ya Afya tunasimamia upatikanaji  wa huduma za afya na haki za wazee na  kupinga ukatili dhidi yao" Alisema Bi. Cecilia


Katika maadhimisho hayo yaliyofanyika kiwilaya Halmashauri ya Mji wa Mbinga, wazee waliweza kupata huduma  za afya ikiwemo kupima na kupata msaada wa kisaikolojia.


Maadhimisho yalitanguliwa na kongamano lililofanyika Septemba 30, 2023 katika Ukumbi wa mikutano wa Oddo Mwisho.


Katika kongamano hilo wadau walijadili mambo yahusuyo mmomonyoko wa maadili, ukatili dhidi ya wazee, malezi na namna bora ya kutatua changamoto zinazowakabili wazee.

Matangazo

  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA June 04, 2025
  • TANGAZO LA KAZI August 07, 2024
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2023 December 14, 2022
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2022 January 04, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kheri ya Siku ya Mazingira Duniani

    June 05, 2025
  • Utoaji wa dawa za minyoo na vitamin A kuanza Juni 1 Mbinga Mji

    May 31, 2025
  • MBINGA MJI YAFANYA TATHIMINI YA LISHE

    May 29, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA WAWASILI MBINGA MJI

    May 26, 2025
  • Tazama zote

Video

MAONYESHO YA NANENANE 2023 MBINGA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.