English
  • English
  • Kiswahili
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga Town Council
Mbinga Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

WATUMISHI WA HOSPITALI YA MBUYULA WATAKAOKIUKA MAADILI YA KAZI YAO KUCHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA

Tarehe ya kuwekwa: September 21st, 2023


Na Alex Nelson Malanga


Afisa Habari---MTC


Mbinga.  Uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga (MTC) umetoa onyo kali kwa watumishi wa  Hospitali ya Halmashauri hiyo (Mbuyula) kutojihusisha  na vitendo vya rushwa au vitendo vingine ambavyo ni kinyume na maadili.



Onyo dhidi ya watumishi hao lililotolewa Septemba 19, 2023 wakati wa mkutano kati ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mbuyula, viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambambana na Rushwa (TAKUKURU) pamoja na watumishi wa Hospitali hiyo.    


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Bi. Amina Seif  alisema kama kuna watumishi wanaomba rushwa kwa watu ili wapewe huduma kwa haraka waache tabia hiyo ili kulinda taswira nzuri ya Hospitali.



 Aliwataka watumishi wajikite kwenye kuboresha huduma zao huku wakizingatia maadili ya kazi yao.


"Kazi hii ni ya wito, mnapaswa kuwa waadilifu, vinginevyo sheria itachukua mkondo wake kwa watakaobainika kujihusisha na vitendo visivyo vya kimaadili,” alionya Bi. Amina.


Afisa wa TAKUKURU Blandina Hamisi alisema taasisi yao iko kazini na kwamba watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria.


Alisema ni vizuri kuzuia rushwa ili wasifikie hatua ya kupambana na adui huyo ambaye ni kikwazo cha maendeleo.


“Wengi wetu tunatokea familia za kimaskini. Familia zinatugemea. Jamii inatutegemea,” alisema Bi. Blandina.


Aliongeza: “Fanyeni kazi kwa uadilifu ili mstaafu vizuri.”


Afisa TAKUKURU mwingine Ibrahim Magoti aliwataka watumishi wa umma kutumia elimu yao kutoa huduma bora huku wakizingatia maadili ya kazi zao.


“Tutoe huduma bila upendeleo. Tufuate kanuni na taratibu za Hospitali,” alisema Bw. Magoti.


Aliwataka watumishi kutoa taarifa kuhusu wenzao watakaojihusisha na vitendo vya rushwa.


“Mchuma janga hula na wa kwao. Kwahiyo tusilindane kwani ukiwalinda waovu inaweza kukurudia,” alisema Bw. Magoti.


“Ukiona mwenzako hana uadilifu, mwambie abadilike na ikiwezekana toa taarifa kwa uongozi ili tusichafue taswira ya Hospitali.


“Mtumishi wa umma ni kioo cha jamii hivyo tunapaswa kuwa waadilifu kwa kuwajibika kwa umma huku tukifuata sheria.”

Matangazo

  • TANGAZO LA MAPOKEZI YA FEDHA March 20, 2025
  • TANGAZO LA KAZI August 07, 2024
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2023 December 14, 2022
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2022 January 04, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE WA UHURU WAWASILI MKOA WA RUVUMA

    May 10, 2025
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Halmashauri ya Mji wa Mbinga Tarehe 13 Mei 2025

    May 06, 2025
  • Huduma za Dawati la Msaada wa Kisheria Halmashauri ya Mji wa Mbinga

    May 05, 2025
  • JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA WILAYA MBINGA YAOMBA HALMASHAURI YA MJI MBINGA KUBORESHA VIBANDA SOKO LA MISHENI

    April 28, 2025
  • Tazama zote

Video

MAONYESHO YA NANENANE 2023 MBINGA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.