• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Government Web Framework

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Government Web Framework

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

WAZIRI WA UTAMADUNI AWATAKA WANANCHI WA MBINGA KUENZI MILA NA DESTURI

Tarehe ya kuwekwa: October 31st, 2023



Na Rahma Mwaka, Elizabeth Newa & Erasto George


Mbinga. Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema utandawazi umekuwa ni chanzo kikubwa cha mmomonyoko wa maadili kwa kuwa baadhi ya jamii za kitanzania zimeacha kufuata mila na desturi zao.


Katika muktadha huo, aliwataka wamatengo na wananchi wote wa Mbinga kwa ujumla kuendelea kuzilinda na kuzienzi mila na desturi zao ili ziendelee kuwepo siku zijazo.



Mhe. Dkt.  Ndumabaro aliutoa wito huo jana Oktoba 30, 2023 katika tamasha la siku ya wamatengo lililofanyika katika kijiji cha Mtama, kata ya Utiri, ambapo alikuwa mgeni rasmi.


"Jamii isiyokuwa na utamaduni ni jamii mfu, hivyo ninalipongeza Baraza la Makumbusho kwa kuandaa tamasha hili kwa kuwa linalenga kudumisha na kurithisha utamaduni kwa kizazi hiki na kijacho,” alisema Mhe. Dkt. Ndumbaro.


Alimwagiza mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Bi. Amina Seif kujenga jengo la Makumbusho ya wamatengo katika kijiji cha Mtama, kata ya Utiri ambapo walifanyia tamasha hilo kwa mwaka huu.


“Tamasha hili liendelee kufanyika hapa kwa kuwa ndio asili ya wamatengo na itakuwa chanzo cha utalii pamoja na kukuza utamaduni wa kimatengo,” alisisitiza Mhe. Dkt. Ndumbaro.  


Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Aziza Mangosongo alisema wazee wa Baraza la Makumbusho wanastahili pongezi kwa kuwa wametambua umuhimu wa kudumisha mila na desturi za kimatengo.


“Chama cha Mapinduzi kinatambua mila na desturi katika ilani yake hivyo viongozi tunatekeleza ilani ya chama kwa kushirikiana nanyi katika shughuli kama hii,” alisema Mhe. Aziza.


Mwenyekiti wa Baraza la Makumbusho (Mbinga) Bw. Osmund Kapinga alisema vijana wamekuwa wakidharau mila na desturi ambapo hupelekea mmonyoko wa maadili.


Aliwashauri vijana ambao bado wapo shuleni kusoma masomo ya sayansi ili waweze kubuni zana za kisasa na kuondokana na zana za jadi ambazo hutumika katika kilimo.

Matangazo

  • KUITWA KATIKA USAHILI October 13, 2025
  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI May 25, 2022
  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA June 04, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 13, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kambi ya madaktari Bingwa wa Dkt Samia Suluhu Hassan yaendelea kutoa Huduma Halmashauri ya Mji Mbinga

    September 24, 2025
  • KISHINDO CHA MHE.RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN MBINGA MJI KATIKA MIRADI YA ELIMU

    August 29, 2025
  • KISHINDO CHA MHE.RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN MBINGA MJI KATIKA MIRADI YA ELIMU

    August 29, 2025
  • KISHINDO CHA MHE.RAIS,DKT. SAMIA SULUHU HASSAN MBINGA MJI KATIKA MIRADI YA ELIMU

    August 29, 2025
  • Tazama zote

Video

MAONYESHO YA NANENANE 2023 MBINGA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Government Web Framework

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki