• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Mji Mbinga

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

MBINGA YAFUNGUA FURSA MPYA ZA UWEKEZAJI

Tarehe ya kuwekwa: January 17th, 2026

MBINGA, RUVUMA: Wilaya ya Mbinga imetangaza mkakati mpya wa kukuza uchumi wake kupitia uwekezaji wa viwanda, maghala ya kisasa ya kuhifadhia chakula, na ujenzi wa makazi bora, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya kuimarisha sekta ya biashara nchini.

Mkakati huo umebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Mhe. Kisare Makori, wakati akiongoza Kikao cha Baraza la Biashara la Wilaya hiyo kilichohusisha viongozi wa Halmashauri zote mbili (Halmashauri ya Mji Mbinga na Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga) pamoja na wadau wa sekta binafsi. Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya tarehe 16 Januari 2026.

Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Makori amesema Wilaya imejipanga kikamilifu kwa kutenga maeneo maalum ya uwekezaji katika Kata ya Kitanda (Halmashauri ya Mji) na Maguu (Halmashauri ya Wilaya), ambapo viwanja kwa ajili ya viwanda na taasisi vimeanza kuandaliwa kwa ajili ya kuuzwa kwa wawekezaji.

"Tunapiga hatua kubwa kwenye miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri zetu, lakini lengo letu kuu ni kuhakikisha maendeleo haya yanaenda sambamba na kuweka mazingira rafiki ya kufanya biashara na uwekezaji ili kufikia malengo ya kitaifa," alisema Mhe. Makori.

Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya amewahimiza watendaji wa Halmashauri kuhakikisha wanatatua kero ndogo ndogo zinazowakabili wafanyabiashara ili kuongeza thamani ya uwekezaji wilayani humo. Amebainisha kuwa kuimarika kwa maghala ya chakula na viwanda kutasaidia wakulima wa Mbinga kuongeza thamani ya mazao yao na kupanua soko.

Kwa upande wao, Wakurugenzi wa Halmashauri hizo wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mji Mbinga, Bw. Maurusi Ndunguru, wameahidi kufanyia kazi changamoto zote zilizoibuliwa na Baraza la Biashara ili kuhakikisha miradi mipya inayotekelezwa inaleta tija ya haraka kwa wananchi.

Nao wawakilishi wa wafanyabiashara na wadau wa maendeleo wameishukuru Serikali kwa hatua hizo, wakieleza kuwa upatikanaji wa viwanja vya uwekezaji na ujenzi wa maghala utachochea kasi ya ukuaji wa biashara na kuongeza mzunguko wa fedha ndani ya wilaya hiyo inayosifika kwa uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.

Mbinga sasa inatajwa kuwa moja ya wilaya zenye fursa kubwa mkoani Ruvuma kutokana na mipango yake ya kugawa maeneo ya makazi na viwanda yanayofikika kwa urahisi, jambo linalotajwa kuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Matangazo

  • KUITWA KATIKA USAHILI October 13, 2025
  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI May 25, 2022
  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA June 04, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 13, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBINGA YAFUNGUA FURSA MPYA ZA UWEKEZAJI

    January 17, 2026
  • MKUU WA IDARA MAENDELEO YA JAMII AHAMASISHA VIKUNDI KUJISAJILI- MBINGA MJI

    January 15, 2026
  • MAFUNZO YA MFUMO WA MANUNUZI WA UMMA NA MATUMIZI YA MODULI MPYA KWENYE MFUMO WA NeST KWA MAKUNDI YA VIJANA, WANAWAKE, WAZEE, WATU WENYE ULEMAVU NA WAZABUNI

    January 15, 2026
  • NAIBU WAZIRI KWAGILWA ARIDHISHWA NA UJENZI WA BARABARA YA UTIRI, MBINGA MJI

    January 11, 2026
  • Tazama zote

Video

MKUU WA WILAYA YA MBINGA AHITIMISHA MAADHIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Halmashauri ya Mji Mbinga

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki