• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga Town Council
Mbinga Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

Msimu mpya wa Kahawa 2018/2019 Wilayani Mbinga wafunguliwa rasmi

Tarehe ya kuwekwa: June 30th, 2018

Mkuu wa wilaya ya Mbinga Ndg. Cosmas Nshenye amefungua rasmi msimu mpya wa uuzaji wa zao la Kahawa Wilayani Mbinga tarehe 29/06/2018. Katika ufunguzi huo Mhe. Mkuu wa wilaya alieleza kuwa msimu huu umetoa fursa kwa Wakulima kuuza zao la Kahawa kupitia vyama vyao vya Msingi (AMCOS).

Akihutubia wadau mbalimbali wa kahawa na viongozi wa vyama vya msingi Mhe. Mkuu wa wilaya ya Mbinga alisema kuwa uuzwaji wa zao la kahawa kupitia Ushirika kwa msimu huu ni kutekeleza maagizo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) kwamba Wakulima wote wa zao la kahawa lazima waunde vikundi (AMCOS) na kahawa yao itatoka kwenye hizo AMCOS kwenda kuuzwa mnadani kupitia chama  kikuu cha Ushirika, hii ni kutekelezwa kwa ilani ya chama 2015 chini ya uongozi wa Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe  Magufuli.

Mkuu wa wilaya aliwaasa wakulima wa kahawa kuwa ni lazima kahawa ikusanywe na kutunzwa vizuri kwa kiwango chenye ubora ili kuweza kujipatia soko nzuri litakaloweza inua pato lao na Taifa kwa ujumla ili kufikia maisha bora ambapo mkulima anaweza kujipatia stahiki (mahitaji) mbalimbali bila wasiwasi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Ndg. Robert K. Mageni aliahidi kufanya usimamizi na kudhibiti utoroshaji pamoja biashara isiyo rasmi (Magoma) kwa zao la kahawa ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa vyama vya Msingi kupitia wataalamu husika wa kilimo ili kuona utekelezaji wa agizo la Wazili Mkuu linafikiwa.

Kwa namna ya pekee,  Viongozi wa vyama vya Msingi walipendekeza Taasisi za Kifedha kuwapatia Fedha kwa wakati ili waweze kukidhi mahitaji yao kijamii ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa pembejeo kwa lengo la kuboresha mazao yao shambani.

Kutokana na sensa iliyofanyika baada ya agizo la Waziri Mkuu, Wilaya ya Mbinga ina jumla ya wakulima wa zo la kahawa takribani 12,146 ambao wanajumla ya Hekta 7973.24 na wana jumla ya AMCOS- 14  kwa Mbinga Mji na chama Kikuu kimoja cha Ushirika MBIFACU. Makisio ya uzalishaji wa kahawa kwa msimu 2018/19 ni zaidi ya Tani 3,000.

Akifunga kikao hicho cha ufunguzi wa msimu, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Ndg. Ndunguru Kipwele aliwataka viongozi  hao kuimarisha Ushirika ili kuwa na nguvu kama miaka ya zamani ili kuachana na ubadhilifu uliosababisha Chama Cha Ushirika MBICU kufilisika. Hivyo kuwa na Ushirika wenye nguvu utakuwa ni Mkombozi kwa Mkulima wa Mbinga.

Matangazo

  • TANGAZO LA MAJIBU YA USAILI WA UDEREVA MAFUNZO KWA VITENDO June 20, 2025
  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI May 25, 2022
  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA June 04, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 13, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MBINGA MJI APATIWA TUZO

    June 20, 2025
  • MKUTANO WA JUKWAA LA MWAKA LA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI WILAYA YA MBINGA

    June 20, 2025
  • ‎MBINGA MJI YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI

    June 19, 2025
  • ‎JAMII YAHIMIZWA KULINDA HAKI ZA WATOTO

    June 16, 2025
  • Tazama zote

Video

MAONYESHO YA NANENANE 2023 MBINGA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.