BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Mbinga Mji Mkoani Ruvuma limempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi. Grace Stephen Quintine pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Ndg. Cosmas Nshenye kwa kuwatunuku vyeti ikiwa ni sehemu ya kutambua kazi bora zinazofanywa na wakuu hao za kuendeleza Halmashauri hiyo.
Akiwatunuku Vyeti hivyo kwenye kikao cha baraza la Madiwani ,Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Ndg. Kelvin Mapunda amesema kuwa Madiwani kwa pamoja wametambua kazi zinazofanywa na wakuu hao na kuamua kuwatunuku vyeti hivyo ambavyo vitakuwa ni kumbukumbu katika maisha yao.
Akizungumza kwenye kikao cha baraza hilo ambacho kimehudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Mbinga mjini Jonas Mbunda pamoja na waalikwa mbalimbali viongozi wa chama na Serikali na wakidini akiwemo Askofu wa Jimbo la Mbinga mhashamu John Ndimbo, Mwenyekiti Mapunda amesema kuwa licha ya kuwatunuku vyeti hivyo lakini bado Madiwani hao wamewapatia wakuu hao kila mmoja kiwanja cha kujenga makazi (Nyumba) .
MBINGA
Sanduku la Barua: P.O.BOX 135
Simu ya Mezani: +225 - 2640664
Mobile: +225 – 2640664
Barua pepe: td@mbingatc.go.tz
Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.