Wananchi wa kijiji cha mbangamao kata ya Mbangamao Halmashauri ya Mji wa Mbinga, wametakiwa kuacha tabia ya kuwashawishi watoto wafanye vibaya katika mitihani yao ya mwisho ili wasiendelee na masomo kwa maslahi yao binafsi . Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe Aziza Ally Mangosongo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo na baadae kusikiliza changamoto zinazo wakabili wananchi katika kata hiyo.
Katika ziara hiyo Mkuu huyo wa Wilaya alitembelea na kukagua Miradi mitatu ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa kituo cha afya Mbangamao, Bweni la wanafunzi Sekondari ya Mbangamao na ujenzi wa vyumba vya mawili madarasa shule ya msingi Mbangamao na kusisitiza umakini wa usimamizi katika utekelezaji wa Miradi hiyo.
Akisisitiza suala la elimu Mhe Mangosongo amesema ili kupata matokeo mazuri katika kata, ni lazima wazazi wakishirikiana na Serikali kuwasimamia watoto katika masomo na mienendo yao ili kubaini mapema changamoto zinazoweza kuwakabaili na kuzipatia ufumbuzi. Hata hivyo amewataka wazazi kuhakikisha watoto ambao hawako katika bweni kuhamia katika bweni, ili kupunguza changamoto mbalimbli wanazoweza kuzipata zikiwemo za kitaaluma na hata unyanyasaji wa kijinsi hususani watoto wa kike.
Sambamba na hayo Mkuu huyo wa Wilaya amewasistiza wananchi kujitokeza tarehe 23 mwezi wa 8 kuhesabiwa katika Sensa ya watu makazi. Hata hivyo Mhe Mangosongo amewapongeza wananchi wa kata hiyo kushiriki kikamilifu katika zoezi la Anwani za makazi na postikodi kwakua nyumba zote sasa zimepatiwa namba hivyo itarahisisha zoezi la Sensa ya watu na makazi
Kwaupande mwingine Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wananchi hao kuzingatia lishe bora ili kuepuka udumavu, kuwapeleka watoto kuanzia miaka 0 hadi 5 katika chanjo ya polyo ili wasipate ugnjwa wa kupooza, sambamba na watu kushiriki chanjo ya Uviko-19.
Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo Mhe Bosco Luoga amemshukuru Mhe; Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea wananchi wa kata Mbangamao mradi mkubwa wa maji wa kiasi cha Bilion moja na milioni mianane na kusema katika kuhakikisha tunamtua mama ndoo kichwani wananchi wa kata ya Mbangamao wamefarijika sana. Kwa upande mwingine Mhe Bosco amemshuru Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi Grace Quintine kwa ushirikiano mkubwa wa wataalamu ngazi ya Halmashauri katika utekelezaji wa miradi mbalimbali inayoendelea katika kata yake.
Na Makangury
MBINGA
Sanduku la Barua: P.O.BOX 135
Simu ya Mezani: +225 - 2640664
Mobile: +225 – 2640664
Barua pepe: td@mbingatc.go.tz
Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.