Mwenyekiti wa kamati ya siasa Ccm Mkoa Ndg Oddo kilian Mwisho ametoa maelekezo kwa watendaji wa kata na kijiji Mkoa wa Ruvuma kuandika taarifa na kuzibandika kila hatua ya matumizi ya fedha katika miradi inayo tekelezwa katika maeneeo yao nakubainisha kiasicha fedha kilicho tolewa na wahisani,nguvu za wananchi pamoja na Serikali ili kuwapataarifa sahii wanachi juu ya miradi inayo endelea katika maeneo yao .Mwekiti huyo, ameyasema hayo Wilayani mbinga halmashauri ya mbinga mji kata ya kagugu alipokukuwa akikagua mradi wa ujenzi wa zahanati.
Kamati hiyo imaeridhishwa na kwa kiwango kikubwa na usimamizi mzuri wa miradi hiyo ya maendeleo inayo simamiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi Grace Quintine pamoja na timu yake wakuu wa idara na vitengo katika Halmashauri hiyo. Ataivyo kamati imeendelea kutoa maagizo na kuwaomba watendaji na wanachi kumpa ushirikiano Mkurugeni huyo na timu yake ili kuweza kukamilisha miradi hiyo kwa wakati. Miradi hiyo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule za msingi na Mahabara kwa Sekondari , katika kata tatu Lusonga , Luhuwiko, Mangamao sambamba na ujenzi wa Zahanati katika kata za Luwaita,Kagugu na Masumuni na kikundi cha utengezaji wa chaki cha MORAF, ambapo zaidi ya million 200 zimetumika kutoka mapato ya ndani ,Serikali kuu ,Mfuko wa Jimbo na Nguvu za wananchi .
Nae kaimu katibu tawala wa Mkoa Ndg Joel Mbewa amemwakikishia mwenyekiti huyo kuwa kama Serikari wataweka uataratibu na miongozo kwa wakurugenzi ili kuondokana na chanagamoto, mapungufu yaliojitokeza ili kuweka uwelewa kwa wanachi juu ya utekelezaji wa miradi ya Serikali. kwa upande mwingine Ndg Mbewa amewashukuru wananchi pamoja na serikali kwa kujitoa na kusaidia utekelezaji wa miradi hiyo
Na Makangury.
MBINGA
Sanduku la Barua: P.O.BOX 135
Simu ya Mezani: +225 - 2640664
Mobile: +225 – 2640664
Barua pepe: td@mbingatc.go.tz
Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.