Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Bi Grace Quintine ametembelea kikundi cha Mitenga FFS kilichopo katika kijiji cha Sepukila kata ya kilimani Halmashauri ya Mji wa Mbinga na kukagua shuguli za kilimo cha kahawa zinazofanywa na kikundi hicho. Akisoma risala ya kikundi kwa Mkurugenzi Katibu wa kikundi hicho Ndg Magnus Mbele amesema, pamoja mafanikio waliyo ya pata zipochangamoto za uchache wa wataalamu wa kilimo hususani kata ya kilimani kulingana na ukubwa wa kata na upatikanaji wa pembejeo, hivyo kumwomba Mkurugenzi kuzitazama changamoto hizo kwa namna ya pekee ili kuweza kuzitatua
Kikundi cha Mitenga ni kikundi kinacho jishughulisha na kilimo cha kahawa, ufugaji na bustani ya uzalishaji mbegu na miche ya kahawa, aidha ubia baina ya kikundi na Halmashauri ya Mji wa Mbinga ni hatua kubwa kukiwezesha kikudi kupata mtambo wa kukoboa kahawa katika kata hiyo, ataivyo bado kikundi kinachangamoto ya upungufu wa visima vya kusindika kahawa hiyo pamoja na meza za kuanikia
Kwa upande wake Mkuurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi Gace Quintine amemtaka mkuu wa idara ya kilimo wa Halmashauri Ndg Enock Nduguru kufanya utaratibu wa kuwaeza kupata afisa ugani ili kuwaeza kutatua changamoto ya kitaalamu kwa kikundi hicho.Ataivyo amewataka wanakukundi kuweka mahitaji hayao kwa maandishi na kuwasilisha katika ofisi ya Mkurugenzi ili kusaidi swala la ufuatiliaji na kutatua changamotohizo kwa haraka
Na Makangury
MBINGA
Sanduku la Barua: P.O.BOX 135
Simu ya Mezani: +225 - 2640664
Mobile: +225 – 2640664
Barua pepe: td@mbingatc.go.tz
Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.