• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga Town Council
Mbinga Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

HALMASHAURI YA MJI WA MBINGA YAVUKA LENGO LA UPANDAJI MITI KWA ASILIMIA 6.7

Tarehe ya kuwekwa: February 1st, 2024


Na Alex Nelson Malanga


Afisa Habari---Mbinga TC


Mbinga.  Wakati serikali ikiitaka kila Halmashauri kupanda miti milioni 1.5 kwa mwaka, Halmashauri ya Mji wa Mbinga kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa misitu tayari imevuka lengo hilo kwa asilimia 6.7, ikiwa ni miezi minne kabla ya mwaka huu wa fedha kukamilika.  


Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliwahi kunukuliwa na vyombo vya habari akitoa agizo kwa kila Halmashauri kupanda miti milioni 1.5 kwa mwaka ikiwa ni jitihada za Serikali za kuhakikisha mazingira yanahifadhiwa na kutunzwa.



Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti mashuleni siku ya Jumatano, Januari 31, 2024, Afisa Misitu wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Bw. Sota January Ndunguru alisema tayari Halmashauri kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa misitu, imezalisha miche milioni 1.6.


Uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika katika shule ya Msingi Mkwaya, Kata ya Kilimani, ulihudhuriwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Mhe. Alex Andoya, ambaye alikuwa mgeni rasmi na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Dkt. Kung’e Nyamuryekung’e.


Wengine waliohudhuria ni Mwenyekiti wa kamati ya Mazingira ya Halmashauri ya Mji wa Mbinga Mhe. Amanyisye Ngonepo, wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri na wadau mbalimbali wa misitu na mazingira.


“ Katika mwaka wa fedha 2023/24 Halmashauri ya Mji wa Mbinga kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa misitu imezalisha miche ya miti milioni 1.6,” alisema Bw. Ndunguru, huku akiwataja wadau hao kuwa ni Wakala wa Huduma za misitu (TFS), Mfuko wa Misitu na watu binafsi.


Miche ya miti iliyozalishwa ni ni ile ya matunda, rafiki wa maji, mbao, kivuli na mapambo.


Kati ya miche ya miti milioni 1.6 iliyozalishwa, ya kivuli, mbao na mapambo ni milioni 1.347, matunda 232, 890 na vyanzo vya maji 22, 920.


Mhe. Andoya, kwa upande wake, aliwaagiza walimu wakuu wa shule mbalimbali kutengeza utaratibu wa kila mwanafunzi kumiliki mti wake na kuhakikisha anautunza.


“Hii miti tunayopanda tunapaswa kuitunza. Hatutakiwi kuitelekeza huko mbeleni,” aliagiza Mhe. Andoya ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kilimani.


Kwa upande wake Mhe. Ngonepo ambaye pia ni diwani wa Kata ya Betherehemu alishauri vijiji kutunga sheria ndogondogo ili kuhakikisha miti inatunzwa.

Matangazo

  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA June 04, 2025
  • TANGAZO LA KAZI August 07, 2024
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2023 December 14, 2022
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2022 January 04, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kheri ya Siku ya Mazingira Duniani

    June 05, 2025
  • Utoaji wa dawa za minyoo na vitamin A kuanza Juni 1 Mbinga Mji

    May 31, 2025
  • MBINGA MJI YAFANYA TATHIMINI YA LISHE

    May 29, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA WAWASILI MBINGA MJI

    May 26, 2025
  • Tazama zote

Video

MAONYESHO YA NANENANE 2023 MBINGA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.