Akisoma taarifa fupi kwa Mwenyekiti wa ccm Mkoa, Mkurungezi wa Halmashuri ya Mji wa Mbinga Bi Grace Quintine amesema kiasi cha Million 860 zimepokelewa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa 39 na bweni moja ambapo vyumba vya madarasa 34 kwa ajili ya sekondari, na vyumba vya madarasa vitano kwa ajili ya shule shikizi za msingi. Ata hivyo ameieleza kamati hiyo ya CCM mkoa, marabaada yamapokezi ya fedha hizo Halmashuri iliweza kutoataarifa katika vikao halali vya Halmashauri ikiwemo baraza la madiwani, kutoa maelekezao kwa waalimu wakuu na waalimu wasaidizi, pamoja na waasibu namna ya utekelezaji wa miradi hiyo.
Sambamba na hayo Bi Quintine ameishukuru serikali ya awamu ya tano inayo ongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassani kwa kuendelea kuboresha sekta ya elimu, hususani katika niundombinu ya kufundishia nakujifunzia na kwamba marabaada ya kukamilika kwa madarasa hayo kumetatua changamoto ya upungufu wa madarasa katika shule za sekondari.
Akikagua miradi hiyo Mwenyekiti wa CCM Mkoa Ndg Oddo k. Mwisho amesema kama kamati ya CCM mkoa inawapongeza sana watendaji ngazi ya Halmashuri pamoja na wataalam kwa usimamizi na kukamilisha miradhiyo kwa kiwango kizuri na kuwasii wanafunzi kutimiza wajiwao kwa kusoma na kuyatunza majengo hayo . Atahivyo mwenyekiti huyo amesistiza uongozi wa kila kata kuakikisha katika kila maeneo ya taasisi za Serikali kuwa na hati miliki ili kuepuka migogoro inayo weza kujitokeza hapo baadae. Kwaupande mwingine amewakumbusha wanachi kuwa mwakahuu ni mwaka wa sensa ya watu na makazi hivyo wajitokeze kwa wingi ili waweze kuhesabiwa
Na Makangury
MBINGA
Sanduku la Barua: P.O.BOX 135
Simu ya Mezani: +225 - 2640664
Mobile: +225 – 2640664
Barua pepe: td@mbingatc.go.tz
Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.