Zaidi ya shs milioni 400 zimetolewa na Serikali kwa ajili ya mradi wa ujezi wa shule ya sekondari katika kata ya Lusonga Halmashauri ya Mji wa Mbinga, akitambulisha mradi huo kwa wanachi wa kata hiyo, Mkurugenzi wa Halmashuri hiyo Bi . Grace Quintine amesema serikali imetoa kiasi cha shs milioni 600 ambapo kwa awamu ya kwanza serikali itatowa million 470 kwajili ya ujenzi wa shule ya Sekondari katika kata ya Lusonga hivyo kuwaomba wanachi kuupokea maradi
Hata ivyo Bi. Quintine awataka waanchi wa kata hiyo kuupokea mradi huo na kuwapa maelekezo kwa muhutasari namna ya utekelezaji wa mradi huo utakavyo fanyika. Amesema mradi wa ujenzi wa shule hiyo utatumia mfumo wa force Account hivyo wanachi wawe tayari katika shirikiana na kuwa kuunda kamati mbalimbali za usimamizi wa mradi huo. Kushiriki kama nguvu za wananchi kwa kuchimba msingi ,kusogeza mawe, na waakina mama kuakikisha maji yana patikana eneo la mradi ili kuweza kumaliza mradi kwa wakati
Bilioni 130.5 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa shule za sekondari 225 kupitia mradi wa kuboresha elimu ya sekondari nchini (Sequip). Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imepeleka kiasi cha Shilingi Bilioni 100.58 kwa ajili ya ujenzi wa shule za sekondari mpya 214 ambazo zitajengwa kwenye Kata za majimbo yote nchini, na Shilingi Bilioni 30 zimepèlekwa kwa ajili ya ujenzi wa shule za sekondari mpya za wasichana kwenye Mikoa 10 (shule 1 kila mkoa) Tanzania Bara. Katika shule za kata Madarasa nane yatajengwa, Maabara za sayansi tatu, Jengola utawala moja, Maktaba moja chumba ICT kimoja. Vyoo vya wanafunzi (Wav 10 &, Was 10) Tank la Maji lita 10,000 Nguzo ya kuweka Tanki Ujenzi wa Miundombinu ya kunawa mikono Miundombinu ya Kuvuna/ Kuunganisha Maji
Mradi huu wa SEQUIP unatekelezwa kwenye eneo la Elimu ya Sekondari kuanzia Kidato cha 1 – 6 kwa muda wa miaka mitano (5) kuanzia mwaka wa fedha 2020/21 – 2024/25 na utekelezaji wake umeelekezwa kwenye maeneo ya vipaumbele vya Serikali yanayogusa moja kwa moja elimu ya sekondari ambayo ni pamoja na ujenzi wa shule mpya za sekondari zipatazo 1,000 zitakazojengwa katika kata ambazo hazina shule za sekondari na maeneo ambayo yana wanafunzi wengi ukilinganisha na miundombinu iliyopo na ujenzi wa shule mpya za sekondari za wasichana za Mikoa 26 ambapo katika kila Mkoa itajengewa shule moja. Ujenzi wa shule hizi utakua unafanyika kadri fedha zitakavyokuwa zinapatikana na kwa sasa tunaendelea na uchambuzi ili kujenga shule za nyongeza 20 kwenye Kata zenye msongamano wa wanafunzi.
Kwaupande wake Mbunge wa jimbo la Mbinga Mjini Mhe; Jonas Mbunda ameishukuru serikali kwa kuyatazama majibo kwa jicho lapekee na kuendela kuwapa fedha kwa ajili ya milaradi mbalimbali hususani katika Nyanja ya Elimu hivyo kuwaomba wanachi kuupokea na kusimamia kwa uadilifu mradi huo kwakuwa mradihuo ni wa kwao ataivyo wanachi wa kata hiyo wameonyesha kuupokea mradi huo kwa kwafuraha kubwa sana nakuhaidi kushirikiana ili kuweza kukamilisha mradi huo kwa wakati
Na Makangury
MBINGA
Sanduku la Barua: P.O.BOX 135
Simu ya Mezani: +225 - 2640664
Mobile: +225 – 2640664
Barua pepe: td@mbingatc.go.tz
Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.