Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe Aziza Ally Mangosongo amekutana na kufanya kikao na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya hiyo, Wkuu wa Idara,Taasisi na Wadau mbalimbali kuunda kamati ya maadalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru katika Ukumbi wa Oddo Mwisho uliopo katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga , unaotarajiwa kufika tarehe 4/9/2021.
Akito tathimi ya mbio za Mwenge 2019 Mhe Aziza amesema, kwa mwaka huu Mwenge utapokelewa kiwilaya, hivyo ilikuweza kuweza kupata alama zaidi kulinganisha na Mwaka 2019, hatunabudi kushirikiana kwa pamoja na taasisi wadau mbalimbali ili kuwepo na ufanisi katika mapokezi na hii italeta hamasa kubwa kwa wadau kwa kushirikishwa katika mapokezi hayo.
Atahiyo Mkuu huyo amesisitiza kwa kila kamati kushiriki kikamilifu hususani kamati ya hamasa na idara ya Tehama ikiwa ndio ujumbe mkuu wa Mwenge wa Uhuru mwaka huu “TEHAMA ni msingi wa Taifa endelevu: Itumie kwa usahii na Uwajibikaji”. Kwa upandewake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Bi Grace Quintine amemshukuru Mkuu huyo wa Wilaya kwa kuwa nawazojipya la kuzishirikisha taasisi na wadau mbalimbali itasaidia kupunguza majukumu kwa Halmashauri hizo na kwa wakuu wa idara ambapo awali walikuwa wakilifanya majukumu hayo wenyewe.
Na Makangury
MBINGA
Sanduku la Barua: P.O.BOX 135
Simu ya Mezani: +225 - 2640664
Mobile: +225 – 2640664
Barua pepe: td@mbingatc.go.tz
Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.