• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga Town Council
Mbinga Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mipango Miji na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Mawasilianao na Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ofisi ya Mbunge
  • Miradi
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
    • Inayotarajia kutekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria ndogo
    • Fomu mbalimbali
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Video
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari
      • Agustivo High School
      • Dr. Shein Secondary School
      • Makita Secondary School
      • Luhuwiko Secondary School
      • Mbinga Secondary School
      • Mbambi Secondary School
      • Mikiga Secondary School
      • Mbangamao Secondary School
      • Kikolo Secondary School
      • Kagugu Secondary School
      • Ndela Secondary School
      • Ngwilizi Secondary School
      • LAMATA Scondary School
      • Kindimba Secondary School
      • Lusetu Secondary School
      • Depaul Mbangamao Secondary School
      • Mkwaya Secondary School

TUNAKABILIANA VIPI NA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI

Tarehe ya kuwekwa: November 9th, 2021

Mabadiliko ya tabia nchi ni miongoni wa dhana ambayo si ngeni masikioni na imeonekana kutamkwa sana vinywani mwawatu wengi duniani. Jambo hili si geni hata hapa nchini hususani siku za hivi karibuni matukio kadha wa kadha yamekuwa yakijidhihirisha juu ya hilo. Athari za jambo hili likitokea eneo hili kwa namna moja ama nyingine tunakuwa na athari kubwa ambayo ulimwengu mzima zinatokea. Ikumbukwe kwa wakati ule ule tumekuwa hatujui nini chanzo? Nini kisababishi cha tatizo? ambapo kwa haraka haraka majibu ni kwamba kutokuwepo kwa elimu na namna stahiki, (Environmental Communication and Environmental awareness) ya kuweza kukabiliana/kuzuia na kuepukana na janga hili la mabadiliko ya tabia ya nchi,(Climate Change) pili tukumbuke kuwa mabadiliko ya hari ya hewa au mabadiliko ya tabia ya nchi yanahatarisha uwepo wa maisha ya wanadamu na viumbe hai wengine moja kwa moja.

Ukubwa wa tatizo hili unaoambatana na athari unaojumuisha wale wote wanaojiusisha na masuala ya Mazingira/Wanaharakati wa mazingira,(Environmental Managers),hata wale ambao hawajihusishi nayo moja kwa moja. Ingawaje wengi wetu, pengine tumekuwa tukifanya hivyo bila kujua maana ya athari, mbinu stahiki za kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi, nitajaribu kuchambua japo kidogo sana katika makala hii ambayo inaeleza kiundani zaidi juu ya mabadiliko ya hari ya hewa ni jambo lisilowezekana kwa mtu kutojua nini?,chanzo cha tatizo hili na upi ni ufumbuzi wa tatizo hilo kwa kuwa dhana hii ni pana sana katika maisha halisi ya binadamu, ingawaje imepigiwa sana kelele na viongozi wengi, juu ya udhibiti wa swala hili kwa lengo la kurudisha mazingira ya dunia yetu kama yalivyo kuwa hapo awali.

Ikumbukwe kuwa mabadiliko ya tabia nchi yamesababishwa na yanaendelea kusababishwa na shughuli za mwanadamu kwa kutekeleza mipango ilokusudiwa kuchagiza maendeleo ya kiuchumi nchi nyingi ulimwenguni zimekuwa zikitekeleza na kuweka kipaumbele shughuli za maendeleo bila kutilia maanani uwezekano na kuwepo kwa athari za mazingira kwa kizazi cha sasai na kizazi kijacho.

Shughuli za binadamu, zimekuwa ni sababu kubwa sana zinazosababisha “Mabadiliko ya tabia nchi” uandaaji wa mashamba makubwa unapelekea ukataji holela wa misitu, kubadilisha uhalisia wa eneo la misitu kuwa jangwa, shughuli za viwanda, shughuli za kilimo na nyingine nyingi, uunguzaji wa nishati inayotokana na mabaki ya viumbe hai, kama vile petroli, dizeli, makaa ya mawe na gesi asilia na kwa upande mwingine ongezeko la joto duniani ni jambo linalosababishwa na muwako wa nishati kama vile petroli, dizeli, gesi asilia, makaa ya mawe, kuni, na kadhalika kuoza kwa mboji katika maziwa na mashamba ya mpunga na utoaji wa hewa za ukaa kutoka katika mbolea za viwandani, viwanda na vyombo vya usafiri,nishati asilia inapochomwa huzalisha gesi joto ambayo huenda angani na kutuama/kuelekea katika sehemu ya anga hii husababisha kuongezeka kwa joto duniani na kitaalamu inafahamika kama (Global Warming).Hivyo kuna uhitaji mkubwa wa kupunguza uzalishaji gesi joto duniani.

Ukweli unajidhihirisha kwa matukio kadhaa, ambayo yanatokea siku hadi siku hususani kwa mazingira ya mikoa ya nyanda za juu kusini ikiwepo Ruvuma, Njombe, Iringa na Mbeya, ukweli wenyewe ni huu, mnamo miaka ya (1980’s) hari ya hewa katika mikoa hii ilikuwa ni tofauti sana, ukilinganisha na hari tunayoiona sasa ukilinganisha na wakati huo.Vilevile ukame, mvua zisizotabirika, mafuriko, mkondo wa joto kali na kuongezeka kwa vimbunga vikiwepo katrina, rita na vingine vingi, ongezeko la joto duniani, kuongezeka kwa kasi ya kuyeyuka kwa barafu na kubadilika kwa uoto na maumbile asilia duniani.

Harikadharika tasmini ya mwaka (2000’s), iliyofanywa na “Thomson” kutoka chuo cha utafiti wa theruji cha “Byrd” kilichopo “Ohio State Unversity”, (OSU) alisema kiwango cha theruji inayofunika mlima Kilimanjaro hasa katika vilele vyake vya Kibo na Mawenzi. Theruji imeonekana kupotea zaidi na zaidii mwanzoni mwa mwaka,(2007). Takwimu hizo zimejaribu kuonyesha sababu zinazopelekea uyeyukaji wa theruji kwa miaka ya hivi karibuni. Utafiti umebaini kati ya mwaka (1912) hadi (1953), theruji hiyo imepungua kwa kiwango cha (1.1%) kila mwaka hata hivyo kadri miaka inavyozidi kwenda mbele na ongezeko hilo linakuwa kwa asilimia (1.4%) sambamba na hilo chuo cha utafiti cha Marekani, “National Academy of Science”, (NAoF) hakikuwa nyuma kuzungumzia swala hili, hayo yote ni baadhi ya majibu kamili yasiyo hitaji maswali juu ya mabadiliko ya tabia ya nchi.

Takwimu kadhaa zimeonesha chanzo kikuu cha uzalishaji wa gesi ya ukaa ni kutoka nchi zenye maendeleo ya viwanda vikubwa kwa nchi za Ulaya, China, India na Marekani zimechangia na zinaendelea kuchangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya tabia nchi kutokana na kuongezeka kwa kiasi kikubwa cha gesi joto zinazozalishwa kutoka viwandani na katika sekta ya usafiri. Nchi zinazoendelea kutoka bara la Asia, Afrika, Carribean na Amerika ya kusini. Athari hizo zinaathiri mazingira, kiuchumi na kijamii pia kwa mantiki hiyo, sote kwa pamoja inatulazimu kutafuta ushauri wa kitaalamu na kupitia tafiti mbalimbali na kuweza fanyia kazi ili kuweza kutekeleza hatua ambazo zitapelekea kupunguza au kuzuia hali hii. Kwan chi masikini zinachangia kwa kiasi kidogo sana ambapo ni asilimia kumi na saba 17% tu ndio inazalishwa na nchi zinazoendelea kutokana na kupotea kwa misitu kunakotokana na uvunaji holela hivyo wana Ruvuma, Njombe, Iringa, Mbeya inakuwa sijambo jema kwa sisi kuwa ni moja ya wachangiaji katika kuvuna misitu kiholela ikiwa tumekwisha fahamu nini chanzo cha tatizo kwa nchi zinazoendelea.

Harikadharika bara la Afrika linachangia asilimia tatu (3%) tu ya gesi joto inayozalishwa duniani. Ijapokuwa nchi zinazoendelea zinachangia kidogo sana mabadiliko ya tabia nchi hususani zile za Afrika ndizo zinazoathirika sana kutokana na athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa upande mwingine nchi tajiri duniani haziathiriki sana ukilinganisha na nchi maskini ikiwa mikoa mbalimbali hapa nchini inathirika vipi?, ikumbukwe kuwa kuna mazao mengi ambayo uzalishaji wake unahitaji baridi kama chai, kahawa, matunda aina kadhaa ikihusisha (apples, matunda damu, pichezi, peazi,parachichi), maua na baadhi ya tasmini inaonyesha kuwa baadhi ya miti mbalimbali imekuwa imetoweka kabisa katika ukanda pwani wa maeneo ya Lushoto, mkoa (Tanga), Luponde ,Lusitu, Lupembe mkoani (Njombe) na Rungwe,mkoa wa (Mbeya) kutokana na ongezeko la joto inatupasa kujiuliza maswali mengi juu ya hili tatizo.

Kutokana na ripoti ya nne ya jopo la wataalamu la umoja wa mataifa linaloshughulikia mabadiliko ya tabia nchi (Intergovermental Pannel of Climate Change),(IPCC) iliyotolewa mwishoni mwaka (2007), imeonesha kuwa kati ya miaka (1970’s) mpaka (2004’s), Ongezeko la mlundikano wa gesijoto angani umeongezeka kwa asilimia (70%) hivyo wastani wa joto duniani umeongezeka kwa digrii za sentigredi (0.74) toka mnamo mwaka (1800’s) ama katikati ya karne ya kumi na tisa ambapo baada ya mapinduzi ya viwanda kuanzishwa.

Kuwepo kwa ongezeko hili umeleta baadhi ya athari mbalimbali, nazo ni kuongezeka kwa ukame duniani ambayo yameathiri upatikanaji wa chakula kwa binadamu na wanyama, harikadharika imepelekea kushuka kwa uzalishaji wa mazao ya kilimo yanayotegemea mvua kwa asilimia (50%,) kuongezeka kwa matukio ya mafuriko makubwa ambayo yameathiri mifumo hai na kusababisha vifo vya watu na wanyama, kumetokea vipindi virefu vya joto kali na ukame vilivyopunguza upatikanaji wa maji safi kwa kunywa,kumetokea moto hatari iliyoteketeza misitu ambayo mwanadamu anaitegemea kwa nishati kuni, hewa safi (Oksijeni) na uoto wa asili,ongezeko kubwa la magonjwa kama kansa ya ngozi, kipindupindu na mafua pia na kwa upande mwingine magonjwa ya kitropiki kama malaria, dengue, ambayo yamechagizwa na kuongezeka kwa mazalio ya mbu, kutokana na kuongezeka kwa joto, kuyeyuka kwa theluji kwenye safu za milima mirefu, na maeneo yaliyo katika ncha za dunia kunakosababisha kupanda kwa kina cha bahari kutokana na haya jitihada mahsusi na za haraka zinahitajika kuchukuliwa ili kuwakinga na kupunguza visababishi, vya mabadiliko ya tabia nchi.

Utatuaji wake tunaweza tukaangalia mambo kadhaa ikiwemo kuongeza idadi ya upandaji miti, kuacha matumizi ya Chlorofluorocarbon (CFC’s), kupunguza matumizi ya nishati ambayo yatapelekea kuharibu misitu, kutumia nishati mbadala kama gesi, bayogesi, umeme, umeme wa jua (Soral Power) na umeme utokanao na upepo hasa kwa wakazi wa Makambako na maeneo mengine yaliyo na upepo mwingi, naimani itakuwa ni jambo jema sana ikitumiwa njia hii.

Kutokana na ukweli huu hata utatuzi wa jambo hili pia unategemea namna ya kuikabili sababu hii kubwa inayochangia kuwepo kwake. Pongezi nyingi kwa Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya nne Dr. Jakaya Mlisho Kikwete Hasani niliwahi mnukuu akisema haya, “Kwa Mazingira masafi na sayari salama kwa sisi kuishi, ni lazima tuondoe gesi joto kwenye anga, tusimamishe na tupunguze kiwango cha sasa cha utoaji hewa ya ukaa na tupunguze mlundikano wake angani”.

Ni dhahiri kwamba kauli hii ya rais mstaafu awamu ya nne Dr. Jakaya Mlisho Kikwete imelenga kwenye kitovu cha chanzo cha tatizo la “Mabadiliko ya tabia nchi”.Kwa hali hii ni jambo la msingi kujua namna ambavyo gesi joto hasa hewa ukaa ambazo husababisha ongezeko la joto dunia na hatimaye “Mabadiliko ya tabia nchi”, zinavyoweza kupunguzwa.

Sambamba na hilo rais wetu wa awamu ya sita Mh. Samia Suruhu Hasani.hayupo mbali sana na kupambana na harakati za kuifanya jamii ya Tanzania kupingana vikali na ongezeko la mabadiliko ya tabia,(Climate Change) ya nchi, kuna michango mbalimbali ambayo ameifanya na kuonesha dhahili kuwa ni mwanaharakati wa mazingira. Ameweza kuhudhuria mikutano mbalimbali na kuzungumza juu ya mabadiliko ya tabia ya nchi ikiambatana na athari zake.

Jumuia ya Kimataifa kutambua kwamba,kama misitu itajumuishwa katika utatuzi wa “Mabadiliko ya tabia nchi”, hivyo nchi zinazoendelea lazima zifidiwe kwa kuhifadhi na kupunguza ukataji wa misitu unaotokea pale misitu inavyokatwa kwa matumizi mengine ya ardhi hiyo, pamoja na uharibifu wa misitu unaotokea pale maliasili za misitu zinavyoharibiwa. Kwa ardhi yenye misitu inaweza kuwa na thamani kutokana na uuzaji wa mbao uletao fedha za kigeni kwa taifa au uwezekano wa kutumika kwa kilimo cha mazao ya biashara na chakula kwa ajili ya kulisha idadi ya watu inayoongezeka kila siku. Hivyo ni muhimu kutoa tuzo ya fedha ili kuhakikisha kuwepo misitu hiyo kwa kuwapa wananchi hamasa ya kuihifadhi, kuitunza na kuitumia kiuendelevu.

Mchango wa misitu katika kutatua tatizo la “Mabadiliko ya tabia nchi” ni kutokana na ukweli kwamba misitu hufyonza hewa gesi na hivyo kupunguza mlundikano wake angani. Inakadiliwa asilimia ishirini (20%) ya utoaji wa hewa angani unaweza kupunguzwa kwa kutokata na kuharibu misitu. Vilevile misitu inaweza kuchangia katika kukabiliana na “mabadiliko ya tabia nchi” kwa kuipatia dunia huduma ya ikolojia.

Kwa Mawasiliano zaidi na mwandishi wa makala hii 0752 47 47 54 / 0765 19 40 91 au    barua pepe: deodatusmbata@yahoo.com, 

deodatusmbata@gmail.com. cmakangury@gmail.com

 

Na Mbata / Makangury

Matangazo

  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA June 04, 2025
  • TANGAZO LA KAZI August 07, 2024
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2023 December 14, 2022
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2022 January 04, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kheri ya Siku ya Mazingira Duniani

    June 05, 2025
  • Utoaji wa dawa za minyoo na vitamin A kuanza Juni 1 Mbinga Mji

    May 31, 2025
  • MBINGA MJI YAFANYA TATHIMINI YA LISHE

    May 29, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA WAWASILI MBINGA MJI

    May 26, 2025
  • Tazama zote

Video

MAONYESHO YA NANENANE 2023 MBINGA
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Mbinga District Council Website
  • Tunduru District Council Website
  • Madaba District Council Website
  • Nyasa District Website
  • Namtumbo District Website
  • Songea District Council Website
  • Songea Municipal Website

Tovuti zinazohusiana

  • NECTA
  • TAMISEMI
  • AJIRA
  • WATUMISHI PORTAL
  • NACTE
  • PREM

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    MBINGA

    Sanduku la Barua: P.O.BOX 135

    Simu ya Mezani: +225 - 2640664

    Mobile: 0733216557

    Barua pepe: td@mbingatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2021 MBINGA TOWN COUNCIL . All rights reserved.